Kampuni GAPCO Tanzania, imetangaza
kuendelea kudhamini mbio za Kilimanjaro Marathon 2017 za kilomita 10 kwa walemavu.
Akizungumza wakati wa kutangaza udhamini huo jana katika uzinduzi wa mashindano hayo ya
Kilimanjaro Marathon, Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi
alisema Kampuni yake inaona fahari kudhamini mbio hizo za kilomita 10 kwa
walemavu.
“Tumeshuhudia mbio hizi za Kilimanjaro Marathon zikikua tangu tumeanza
kudhamini mwaka wa 2011 na pia kufurahia faida wanayopata wakimbiaji na
jamii inayozunguka maeneo ambayo mbio hizi hufanyika kila mwaka. Tunayo
furaha kufanya kazi na Wild Frontiers ambao ndio waandaaji wa mbio hizi,
Tanzania Paralympic Committee na wizara ya habari, utamaduni, sanaa na
michezo,” alisema Kakwezi.
Alisema kama njia ya kutoa mchango katika sekta ya michezo na kuendelea
kusaidia jamii ambayo GAPCO inafanya biashara, imekuwa mstari wa
mbele katika kudhamini mbio za walemavu na mwakani itagharamia usafiri,
chakula na malazi kwa washiriki kutoka Dar es Salaam na usafiri kwa washiriki
kutoka Arusha. Washindi watapata zawadi zenye thamani ya shilingi milioni 10
kwa ujumla.
“Kakwezi alisema mbio za Kilimanjaro Marathon zimekuwa maarufu na
zinawavutia wanariadha kutoka ndani na nje ya nchi na hivyo zimesaidia sana
kutangaza vivutio vya utalii kama vile mlima Kilimanjaro na kuwaongezea
kipato wafanyabiashara wa mji wa Moshi”.
Tunawathamini wateja wetu ambao mchango wao kwa miaka sita
umetuwezesha kuendelea kudhamini mbio hizi za kilomita 10 hususani kwa
watu wenye ulemavu.
Alisema GAPCO ina matarajio kuwa mbio hizo zitakuwa za kufana na
kuwaomba wateja wao kuendelea kutumia bidhaa na huduma za GAPCO ili
kampuni iendelee kudhamini shughuli kama hizi.
Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (wa pili kushoto) akizungumza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano ya
Kilimanjaro Marathon, iliyofanyika jijini Dar es salaam jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...