Leo Tanzania inaadhimisha miaka 17 toka Baba wa Taifa  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere afariki dunia.Kitaifa maadhimisho haya huambatana na sherehe za kuzima Mwenge na kwa mwaka huu itafanyika katika mkoa wa Simiyu.
 Akiwa mgombea wa Urais mwaka jana Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka shada la maua juu ya kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere huko kijijini Mwitongo, Butiama, mkoani Mara akiwa ameongozana na ujumbe wake.
 Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
 Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiongea na viongozi mbalimbali waliomtembelea Butiama
 Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa na Waziri Mkuu wa India Indira Ghandi pamoja na Rais Kenneth Kaunda wa Zambia, Rais Josef Tito wa Yugoslavia, Milton Obote wa Uganda na Sir Seretse Khama wa Botswana
 Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akikumbatiana na aliyekuwa mgombea Urais Jakaya Mrisho Kikwete baada ya matokeo kutoka na Mhe. Benjamin Mkapa kutangazwa mshindi kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu mwaka 1995.

Kwa makala maalumu ya 
Baba wa Taifa BOFYA HAPA

KUONA TAARIFA MBALIMBALI ZA MWALIMU  BOFYA LINK HIZI:







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Pichani na Kenneth Kaunda, Indira Gandhi, Milton Obote ni Josip Broz Tito wa YUGOSLAVIA sio BULGARIA kama iliandikwa.

    ReplyDelete
  2. DAIMA TUTAKUENZI: (BABA WA TAIFA MWALIM J.K.NYERERE).

    Yote kazi ya Mwenyezi, Nasi sote ndiyo njia,
    Umetutoka kipenzi, Baba wa Watanzania,
    Bado twafuta machozi, Tungali twakulilia
    DAIMA TUTAKUENZI, BABA WA WATANZANIA.

    Miaka 'KUMI NA SABA', Kama leo tadhania,
    Tungali nao msiba, Tama bado shikilia,
    Hakuna wa kuliziba, Pengo ulotuwachia,
    DAIMA TUTAKUENZI, BABA WA WATANZANIA.

    Kulienzi jina lako, Kubwa lililobakia,
    Kuzifata nyao zako, Yakwepa ulochukia,
    Sikiza wosia wako, Hazina ulotwachia,
    DAIMA TUTAKUENZI, BABA WA WATANZANIA.

    DUA njema kuombea, YARABI tuitikia,
    Makosa kusamehea, Waja hatujatimia,
    Memayo lotutendea, PEPONI kesho kutia,
    DAIMA TUTAKUENZI, BABA WA WATANZANIA.

    MOLA akulaze palipo pema Peponi Baba wa Taifa letu la Tanzania, hayati Mwalimu Julius Kambarage NYERERE. AMEN.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...