Mkuu
wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (wa pili kushoto), jana amezindua Meli
mpya na ya kisasa (Kivuko) ya MV NYEHUNGE II yenye uwezo wa kubeba
abiria 500 pamoja na mizigo inayofanya safari zake kati ya Jiji la
Mwanza na Wilaya ya Ukerewe.
“Naamini
kivuko hiki kitakuwa ni mkombozi kwa wakazi wa Ukerewe kwani uhitaji wa
wakazi wa Ukerewe kuhitaji huduma nzuri na salama ya usafiri ni mkubwa
hivyo tunaamini kivuko hiki kitatumika kwa maeneleo ya wanaUkerewe”.
Alisema Mongella na kuongeza kwamba hiyo ni fursa kwa wafanyabiashara wa
Ukerewe kutumia Kivuko hicho katika shughuli mbalimbali za kibiashara.
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (wa pili kushoto), jana amezindua Meli
mpya na ya kisasa ya MV NYEHUNGE II yenye uwezo wa kubeba abiria 500
pamoja na mizigo inayofanya safari zake kati ya Jiji la Mwanza na Wilaya
ya Ukerewe.
Mama
Gertrude Mongella (katikati), akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya
Nyamagana, Bi.Mary Tesha (kulia), pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela,
Dkt.Leonard Masale (kushoto) wakati wa uzinduzi wa Meli hiyo.
“Naamini
kivuko hiki kitakuwa ni mkombozi kwa wakazi wa Ukerewe kwani uhitaji wa
wakazi wa Ukerewe kuhitaji huduma nzuri na salama ya usafiri ni mkubwa
hivyo tunaamini kivuko hiki kitatumika kwa maeneleo ya wanaUkerewe”.
Alisema John Mongella (katikati) na kuongeza kwamba hiyo ni fursa kwa
wafanyabiashara wa Ukerewe kutumia Kivuko hicho katika shughuli
mbalimbali za kibiashara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...