Serikali  imewataka wanawake wachimbaji wadogo wa madini kuwa na umoja ili  kuboresha kazi zao na changamoto zinazojitokeza.
Akifungua mkutano wa kazi wa wadau unojadili namna ya bora ya kuratibu na kuimarisha vyama vya wanawake wachimbaji wadogo wa madini nchini Jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amesema kuwa  serikali inatambua  changamoto zinazowakabilia wachimbaji hao na kuzitaja kuwa ni pamoja na ukosefu wa mitaji, vifaa vya kisasa, teknolojia, elimu ya masoko, uelewa mdogo na ujuzi katika sekta ya madini. 
Hotuba yake ilisomwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Profesa Justin Ntalikwa.
Waziri Muhongo amesema serekali inatambua mchango mkubwa wa wachimbaji hao wadogo katika sekta ya madini  na kueleza dhamira ya serikali ya kuendelea kushirikiana na vikundi na vyama vya wachimba hao wanawake.
Mkutano huo  unajadili matokeo ya  utafiti uliofanywa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji (NEEC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya UN Women Ofisi ya Tanzania.
Katibu Mtendaji wa Baraza hilo,Bi. Beng’i Issa, amesema utafiti umebaini kuwa ushiriki wa wananke katika sughuli au biashara za sekta ya madini ni mdogo  na wachimbaji  wanakabiliwa na changamoto nyingi.
Amesema utafiti umesaidia kuvitambua vyama vya wanawake wachimbaji wadogo wa madini nchini na  kuainisha changamoto wanazokabiliana nazo.
Mapendekezo ya kutoka majadiliano ya mkutano huo yatachukuliwa na serikali kupitia Baraza ilitachukua matokeo ya mkutano huu wa kazi na kuyafikisha serekalini ili yatumike  kwa maendeleo ya sekta madini.
Afisa Miradi Programu ya Kuwezesha Wanawake Kiuchumi wa Taasisi ya Kimataifa ya UN Women, Ofisi ya Tanzania, Bi. Tertula Swai, amesema  sasa hivi kuna ushindani mkubwa wa masoko katika sekta ya madini na kuongeza kwamba utafiti huu umelenga kuwapa elimu wachimbaji  ya kuweza kukabiliana na ushindani huu.
Meneja Mkuu wa Mbalawala Women Organization kutoka Mbinga Mkoani Ruvuma,Bi. Leah Kayombo,amesema shirika lao limefanikiwa kutengeneza mkaa wa kupikia kwa kutumia makaa ya mawe ya Ngaka Mbinga ili ku kupunguza ukataji wa miti kwa ajili ya mkaa.

 Wadau wa sekta ya madini  wakifuatilia majadiliano  juu ya namna  bora ya kuratibu na kuimarisha vyama vya wanawake wachimbaji wadogo wa madini nchini Jijini Dar es Salaam jana. Mkutano huo ni matokeo ya utafiti uliofanywa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji (NEEC) likishirikiana na UN Women, Ofisi ya Tanzania.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kushoto) akifungua mkutano wa kazi wa wadau uliokuwa ukijadili namna ya bora ya kuratibu na kuimarisha vyama vya wanawake wachimbaji wadogo wa madini nchini kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Sospeter Muhongo. (Kushoto) ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng’i Issa na (katikati) ni Mkurugenzi wa Uwezeshaji wa Baraza, Bi Anna Dominick.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa wa pili (kushoto) akimsikiliza Meneja Mkuu wa Mbalawala Women Organization kutoka Mbinga Mkoani Ruvuma,Bi. Leah Kayombo (kulia) Jijini Dar es Salaam jana. Bi Kayombo taasisi yake inatengeneza  mkaa wa kupikia kwa kutumia makaa ya mawe  unaopatikana  machimbo ya Ngaka Mbinga katika jitihada ya kupunguza tatizo la ukataji miti kwa ajili ya mkaa. (Kushoto) ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEE) Bi. Beng’i Issa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kushoto) akibadilishana mawazo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng’i Issa (katikati), mara baada ya kufungua mkutano wa kazi wa wadau uliokuwa ukijadili namna  bora ya kuratibu na kuimarisha vyama vya wanawake wachimbaji wadogo wa madini nchini kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Sospeter Muhongo. (Kulia) ni  Mkurugenzi wa Uwezeshaji wa Baraza Bi. Anna Dominick.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...