Mkurugenzi Mtendaji Godfrey Simbeye akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo wakati wa mkutano wa kuwaandaa watanzania kutumia fursa zilizopo katika ujenzi wa bomba la mafuta ghafi litakalojengwa hapa nchini. 
Mkurugenzi Mtendaji Godfrey Simbeye katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Kushoto ni Meneja Mawasiliano TPDC, Marie msellemo na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Pietro Fiorentini ,Abdulsamad Abdulrahim.

 Na Mwandishi wetu, Globu ya Jamii.
TAASISI ya sekta binafsi Tanzania(TPSF) kwa kushirikiana na Pietro Fiorentini Tanzania kuwaandaa watanzania juu ya fursa zilizopo katika ujenzi wa bomba la mafuta ghafi katika muda mfupi, kati na mrefu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa kutambulisha miradi ya ujenzi wa bomba la gesi jijini Dar e salaam leo amesema kuwa watanzania  na wajasiliamali wadogo na wakati kujiweka tayari kupata fursa zilizopo katika sekta ya mafuta na gesi.

Amesema kuwa lengo la mkutano huu ni kujenga mwamko wa watanzania wenye nia ya kushiriki katika mnyororo huu wa dhamani na kuwapa wauzaji mbinu za kuhudumia mradi huu.

Sembeye amesema kuwa ili kukuza uchumi  na kupunguza umasikini lazima kuwashirikisha wananchi kwa ujumla katika maendeleo ya ujenzi wa bomba la mafuta ghafi hapa nchini.

 Kuhusu jukumu la sekta binafsi katika mradi wa bomba la mafuta amesema kuwa kupitia mitandao ya kibiashara,wafanyabiashara wana weza kubadilishana taarifa na uzoefu na wenzao ndani na nje,mbali ili kujenga mahusiano ya kibiashara.

Sembeye amesema kuwa faida kuu ya Mradi  huo ni pamoja na ujenzi wa bomba la inchi 24 ambalo linatajiriwa kupita katika kilomita 1,403kufikisha mapipa 200,000 ya mafuta yasiosafishwa kwa siku kwa ajili ya mauzo nchi za nje.

Mradi  huo wa shililngi Trilioni 8.7 unatarajiwa kuzalisha ajira 15,000 wakati wa utekelezaji wake baada kukamilika mnamo mwaka 2020,utaweza kuuajiri  watu 1,000 na 2,000.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...