Na Daudi Manongi,MAELEZO.

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa ametoa wito kwa wachimba wadogo wadogo wa madini kuongezea juhudi katika uchimbaji wa madini ikiwa ni pamoja na kujipatia elimu ya uchimbaji sahihi wa madini na kutumia teknolojia nzuri ambayo itawasaidia kuongeza tija katika shughuli zao.

Profesa Ntalikwa ameyasema hayo wakati akifungua mkutano kazi wa wadau wanawake katika sekta ya madini wanaojihusisha na uchimbaji ambao sio rasmi na mdogo uliofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Mimi wito wangu kwa wachimbaji hawa ni kwamba nawaomba wajipatie elimu na teknolojia sahihi ili waweze kujiongezea kipato katika uchimbaji huu”,Alisema Prof Ntalikwa.

Aidha Katibu Mkuu uyo aliwataka wachimbaji wadogo wadogo hao kuwasiliana na Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC) kwa ajili ya kuwasaidia sehemu ambazo ambazo wanaweza kupata mitaji maana suala la mtaji ni muhimu sana ili waweze kuboresha shughuli za uchimbaji.

Pia amesema kuwa serikali imeanza kutoa ruzuku kwa awamu kwa wachimbaji hawa wadogo wa madini na hivi sasa wanajipanga kutoa awamu ya tatu ya ruzuku ikiwa na lengo ya kuwasaidia kununua vifaa vya uchimbaji na teknolojia sahihi itakayorahisisha uchimbaji wa madini na kuongeza kuwa kwa sasa wameshapokea maombi kutoka kwa wachimbaji mbalimbali na wanayafanyia kazi ili wapate washindi watakaojipatia ruzuku.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa amesema kuwa wao kama baraza watatengeneza programu ya jinsi ya kupata uongozi kwa wachimbaji hao ambao utasaidia kuwakilisha mawazo yao serikali na pia program ya kuwajengea uwezo pale ambapo wachimbaji hawa wana mapungufu na pia kuwaunganisha na masoko kama vile viwanda vya ndani ili visinunue malighafi kutoka nje na badala yake wanunue hapa nchini malighafi yanatotokana na uchimbaji wa madini.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof.Justin Ntalikwa na Katibu Mtendaji Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa wakipata maelezo toka kwa Bi Shamsa Diwani wa kikundi cha MIVA kinachojiusisha na uchimbaji mdogo wa madini na usio rasmi leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano kazi wa wadau wanawake katika sekta ya madini.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof.Justin Ntalikwa na Katibu Mtendaji Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa wakipata maelezo toka kwa Bi Susan Fred wa TAMICUSO ambao wanajiusisha na uchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite jijini Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...