Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi(Kushoto),Eng.Stella Manyanya akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam,Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ya Elimu,Prof.Simon Msanjila
Na Chalila Kibuda.
Kozi za foundation katika vyuo zinazotolewa sio mfumo wa Elimu uliopangwa na serikali kumfanya aliyepita kuwa na sifa ya kujiunga na chuo kikuu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Naibu Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya amesema kozi za foundation katika vyuo haijawekewa mfumo ambao unatambulika.
Mhandisi Stella amesema utaratibu huo vyuo vimefanya vyenyewe hivyo serikali haiwezi kuukubali mfumo elimu hiyo.
Amesema anaesoma foundation apewe cheti na kama atahitaji kujiendeleza asafishe cheti au asome mfumo ambao utamfikisha katika shahada.
Amesema suala la watu waliosoma cheti kisha diploma na wakajiunga chuo kikuu hawako sahihi kutokana na vyeti hivyo.Amesema serikali inafanya maboresho ya elimu nchini kutokana na kibaoni vitu vingi ambavyo vimetokana na watu kwenda tofauti na mfumo wa elimu uliowekwa.
Stella amesema wanaendelea kufanya maboresho katika diploma ya ualimu kuweza kuiondoa.Aidha amesema kuwa serikali haitaruhusu elimu kuwa holela kwa watu kuwa tofauti na mfumo uliowekwa.
Pelekeni muswada bungeni iwe sheria hata kama mtaondoka iendelee. la sivyo baada ya miaka 10 tutarudi kulekule kuwapa digrii wasiofaaa mpaka tunapata madaktari wa kuacha visu tumboni na wahandisi wa kuangusha magorofa.
ReplyDeletehata mimi ningekuwa waziri ningetenda hivyo. elimu haina dili wala uchochoro wala mbadala.
ReplyDeleteMaprofessa wanaompinga Ndalichako nao hoi tuuu. Ndo hao walidahili darasa la watu 7000 UDOM. Wanapinga kwa sababu wana midomo.
Ili tuinue elimu yetu ni lazima tuangalie quality assurance.
Big up JPM & Ndalichako (mtawakoma viongozi wasomi wa kweli)
anayetaka kwenda chuo kikuu asome form VI.
ReplyDeletealiyefli form VI arudie mpaka afaulu siyo kupiga dili.
Mbona nafasi za kazi kama jeshi hamna dili? kwamba ambaye si mrefu akivaa stuli atadahiliwa jeshini pia?
ReplyDeleteForm VI haina mbadala. Na waliopata digrii bila form VI wanyanganywe vyeti.
ReplyDelete