Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akikaribishwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Idara ya Polisi ambaye pia ni Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (DIGP), Abdurahman Kaniki (aliyevaa tai) kwa ajili ya kufungua kikao cha Baraza hilo, kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Idara ya Polisi ambaye pia ni Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (DIGP), Abdurahman Kaniki (wapili kulia), Kamishna wa Fedha wa Jeshi hilo, Albert Nyamhanga (kushoto) na Katibu wa Baraza hilo, Merise Mwanyema wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima kabla ya Naibu Waziri kufungua Kikao cha Baraza hilo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Idara ya Polisi (hawapo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya ufunguzi wa kikao cha Baraza hilo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Masauni aliwataka wajumbe hao kufanya kazi kwa vitendo kwa kuyatekeleza ipasavyo maazimio ya kikao hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...