Na Anthony John,Globu Jamii.

Kampuni inayojishughulisha na Uhifadhi wa Mazingira na Usafishaji ya Green WastePro Ltd imesema kuwa, wamejitolea kuiboresha Askari Monument Garden kuwa ya mfano na ya kisasa katika Jiji la Dar es salaam.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja Mwendeshaji wa Kampuni hiyo,Abdallah Mbena leo wakati akizungumza na Globu ya Jamii,amesema wamejitolea kutengeneza Garden hiyo ili kuunga mkono kampeni mbali mbali za Usafi zinazo ongozwa na Rais Magufuli pamoja na Mkuu wa Mkoa.

"Baada ya kuona kampeni mbali mbali za Usafi zinaendelea tukaona njia rahisi ya kuunga mkono kampeni hizo ni kujitolea kuiboresha Askari Monument Garden kuwa ya kisasa katika jiji la Dar es salaam kwa kuunga mkono Serikali ya awamu ya tano," amesema Mbena

Pia Mbena amesema mpaka itakapofika Mwezi wa tatu marekebisho hayo yatakuwa yamesha kamilika na tutakuwa tayari kuzindua.

Amesema kuwa "Watu wenge wamekuwa wakijiuliza maswali kwa nini pamezungushiwa uzio katika Sanamu la Askari Monument Garden lakini ni Kwa sababu tunataka kuiweka kuwa ya kisasa zaidi."
 Maneja Mwendeshaji wa Kampuni ya Green Weste Pro Ltd,Abdallah Mbena akizungumza na Globu ya Jamii Juu ya Uboreshaji wa Monument Garden Leo hii Jijini Dar es salaam.
Picha ya ndani ya ukarabati unavyoendelea wa Askari Monument Garden.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...