Dotto
Charles Heka (13) aliyekuwa Mwanafunzi wa shule ya msingi Lupungu
wilayani Malinyi hatimaye amefufua ndoto zake za kuendelea na elimu ya
sekondari.
Awali baada ya kuhitimu elimu ya msingi tu wazazi wake walimshinikiza na kumlazimisha aolewe pasipo yeye mwenyewe kuridhia kuishi na mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Masenga, kama mme na mke, akielezea kwa uchungu mbele ya Mkurugenzi wa wilaya ya Malinyi ndugu Marcelin Ndimbwa, Afisa elimu wa wilaya Kalagila Silivesta na mwanasheria Sospeter Kalekwa, mwanafunzi Doto Charles Heka anasema,kwakuwa hakupata kuungwa mkono na hata mmoja wa wazazi na ndugu zake alikubali kuoelewa hivyo hivyo.
Baada
ya matokeo kutoka baadhi ya wasamaria wema waligundua kwamba amefaulu
na amechaguliwa kujiunga na shule ya sekondari ya kutwa ya Ngoheranga na
kuamua kutoa taarifa wilayani iliyopelekea mkurugenzi kulivalia njuga
jambo hilo na baada ya kujiridhisha aliweka mtego na jeshi la polisi
lilifanikiwa kumkamata baba wa mtoto na kumchukua mtoto huyo ambaye
mpaka sasa bado yupo chini ya uangalizi wake mkurugenzi na mtoto anaishi
kwa mwalimu, akisubilia kufunguliwa kwa shule .
Mbali na hayo yote pia Mkurugenzi ameamua kujitolea kumsomesha mwanafunzi huyo kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita na amemwomba afisa elimu mkoa amtafutie nafasi ya shule ya bweni huku Ndugu Masenga aliyetoroka akiendelea kutafutwa na jeshi la polisi na kuhakikisha anatiwa nguvuni na sheria kuchukua mkondo wake na kuwa onyo na somo kwa wengine wote wenye mawazo na tabia za namna hizo ndani ya halmashauri yake. Aidha mkurugenzi amewapongeza maafisa elimu, watumishi wa halmashauri hiyo pamoja na wasamaria wema waliotoa ushirikiano na kumnusuru binti huyo. Mungu atawalipa kwa haya mliyomtendea malaika wake Dotto.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...