Zipo namna nyingi
za kuachana kisheria
kwa wanandoa ambao
wanadhani sasa hawawezi kuendelea. Wengi wetu
tunajua zile za
kupitia mahakamani. Zile ni sahihi lakini
upo uwezekano pia wa
kuachana kwa mkataba
maalum bila kuhitaji
kwenda mahakamani.
Aidha yafaa ifahamike
kuwa Kuachana katika
ndoa na kuamua
kuishi nje ya
ndoa ni jambo
la kawaida. Kisheria si
dhambi mwanandoa yeyote
kuona kuwa sasa
hawezi kuendelea kuwa
katika ndoa.
Ni
kwasababu hii hata
sheria ikatambua uwezekano
wa watu kuachana
na halikadhalika ikaweka
utaratibu maalum kwa
walio tayari kwa
hilo.
Tofauti na
kuachana kwa mkataba
namna nyingine ni
kwa njia ya
talaka mahakamani na kwa njia
ya kutengana mahakamani
ambazo nazo tutaziona hapa
chini kabla ya kutizama
ile ya mkataba.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA
Kusoma zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...