Na Humphrey
Shao,
Globu ya Jamii
Kundi la
Waandishi wa habari kumi na Muigizaji mmoja kutoka nchini Israel lililokuja
katika utalii wa maeneo mbalimbali nchini limeondoka leo mara baada
ya kumaliza ziara yao ya siku tano nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini (TTB) Bi. Devotha
Mdachi amesema kundi hilo ambalo lilitembea sehemu mbalimbali nchini limewasili
jijini Dar es Salaam leo kutoka Kigoma na linataraji kuondoka nchini leo majira
ya saa tisa kurudi nchini kwao kwa ndege maalumu ya kukodi.
“Waandishi
hawa wa Habari waliofika kufanya utalii nchini ni moja ya matunda yaliyotokana
na Rais John Pombe Magufuli kurudisha diplomasia baina ya Islael na Tanzania
mara tu walipofungua ubalozi wao hapa nchini hivyo watalii hawa walipata fursa
ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti, visiwa vya Zanzibar na hifadhi ya
Sokwe iliyopo Gombe mkoani Kigoma” amesema Bi. Mdachi.
Kwa upande
wake afisa habari wa Shirika la Hifadhi ya Taifa nchini (TANAPA), Bw. Pascal
Shelutete amesema kuwa watalii hao wamejionea vivutio vingi sana hapa nchini na
kusema kuwa kweli nchi hii inahitaji kuitwa nchi ya Asali na Maziwa kama ilivyo
kwao.
Amesema kuwa
watalii hao wamefuraishwa na jinsi uoto wa asili ulivyo hifadhiwa hapa nchini
na kikubwa zaidi kuona sokwe ambao kisayansi inasemekana kuwa wana mahusiano
makubwa na wanadamu kwa asilimia 98%.
Kwa upande
wake kiongozi wa kundi hilo la watalii hao, Ronit Hershkovitz, amesema kuwa
amefurahishwa sana na vivutio vilivyopo hapa na kwa sasa kundi hilo linakwenda
kuwa mabalozi kwa watalii wengine wanaotoka ukanda wa Magharibi hasa nchi za
Mashariki ya kati.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Bi. Devotha Mdachiakiaga na kiongozi wa kundi la Waaandishi wa habari na watali kutoka nchini Israel Bi. Ronit Hershkovitz kabla ya kuondaka kurudi nchini kwao
Kiongozi wa
kundi la Waaandishi wa habari na watali kutoka nchini Israel Bi. Ronit
Hershkovitz akizungumza na vyombo vya habari vya hapa nchini kabla ya kuondaka kurudi nchini kwao
Afisa Habari Shirika la Hifadhi ya Taifa nchini (TANAPA), Bw. Pascal Shelutete akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam wakati akiagana na kundi hilo la Watalii kutoka nchini Islael
Afisa Habari Shirika la Hifadhi ya Taifa nchini (TANAPA), Bw. Pascal Shelutete akiagana na Kiongozi wa kundi la Waaandishi wa habari na watali kutoka nchini Israel Bi. Ronit Hershkovitz
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...