Katika kufanikisha azma ya kupanua wigo wa huduma za kifedha kwa wananchi wenye vipato tofauti, kampuni ya mawasiliano ya Halotel na benki ya NMB zimeingia katika ushirikiano utakao wawezesha mamilioni ya watanzania kunufaika na huduma za kifedha nchi nzima. 

Hatua hii itawawezesha watanzania wengi zaidi kufikiwa na huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ikiwa ni sehemu ya kufanikisha azma ya serikali ambayo inazitaka taasisi mbalimbali za kifedha kuwafikia wananchi na huduma zao hasa kwa maeneo ya vijijini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel, Bw. Le Van Dai amesema kuwa ni hatua nyingine kubwa katika utoaji wa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi ambapo sasa huduma ya Halopesa itakuwa imeunganishwa na benki ya NMB ili kuwawezesha wateja kufanya miamala kwa urahisi zaidi.

Dai ameendelea kuwa ushirikiano huo, umeunganisha taasisi kubwa zenye wateja wengi na zilizosambaa kwa kiasi kikubwa nchini. Tunatarajia huduma hii itapunguza kadhia kwa watumishi wa taasisi za umma, wakiwemo walimu na watu wa sekta zingine wakiwemo wakulima, wavuvi na wafanya biashara wanaoishi vijijini ambako huduma za kibenki hazijafika kote. Maeneo haya kwa kiasi kikubwa hutegemea njia ya simu za mkononi kuweza kutoa fedha au kuweka kwa njia ya haraka na usalama zaidi.

“Ushirikiano huu ni wa kipekee katika kurahisisha maisha ya watanzania ambao wamekuwa wakipata tabu kupata huduma za kifedha kutokana na maeneo wanayoishi. Sisi kama Halotel hadi sasa tumewafikia watanzania kwa zaidi ya asilimia 95. Hivyo ni dhahiri kwamba wateja watakaojiunga nasi wataweza kutoa au kuweka fedha huko huko waliko kupitia kwa mawakala wetu ambao wameenea nchi nzima,” aliongezea Dai.
 
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu ya Halotel Le Van Dai akitiliana saini hati za makubaliano na Kaimu Mkuu wa Akiba za watu Binafsi wa benki ya NMB, Boma Raballa ambapo wateja wa Halotel watafaidika na huduma za kifedha za Halopesa kwa ataweza kuchukua na kuweka fedha zake kutoka katika akaunti yake ya NMB. Makubaliano hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Afisa Mwendeshaji wa Halopesa, Henry Mavula na kulia ni Meneja wa Huduma za Ziada wa benki ya NMB,Stephen Adili
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Le Van Dai (kushoto) akibadilishana hati za makubaliano na Kaimu Mkuu wa Akiba za watu Binafsi wa benki ya NMB,Boma Raballa ambapo wateja wa Halotel watafaidika na huduma za kifedha ya Halopesa ambapo mteja wa Halotel ataweza kuchukua na kuweka  fedha zake kutoka katika akaunti yake ya NMB. Makubaliano hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam leo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...