Na Veronica Simba – Dodoma.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekataa kusaini ombi la
uhamishaji wa leseni ya uchimbaji wa kati wa madini ya Shaba Namba ML 571/2017
kutoka kwa mtanzania David Stanley Kayongoya kwenda Kampuni ya Mechanized
Minerals Supreme Mining Company Limited inayomilikiwa na raia kutoka China.
Profesa
Muhongo alikataa kusaini leseni hiyo yenye ukubwa wa kilomita za mraba 0.43
katika eneo la Fufu wilayani Chwamwino mkoani Dodoma, baada ya kubaini kuwa
mtanzania anayetaka kuhamishia leseni hiyo kwa Raia wa China, hatanufaika kwa
kiwango kinachoridhisha.
Akizungumza
na wawekezaji mbalimbali wa sekta husika, waliofika Makao Makuu ya Wizara mjini
Dodoma, kwa ajili ya kusainiwa leseni zao za uwekezaji, jana (Mei 15), Profesa
Muhongo alisisitiza kuwa ni lazima wawekezaji katika sekta husika wazingatie
suala la maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla, wakati wanapotekeleza kazi
zao za uwekezaji.
Waziri
Muhongo alimwagiza mwekezaji huyo raia wa China kujadiliana kwa mara nyingine
na mtanzania mwenye eneo husika (David), ili kuhakikisha ananufaika ipasavyo na
uwekezaji huo.
“Ili
niweze kusaini leseni hii, rudini mezani, mzungumze na kukubaliana ili David
aweze kunufaika. Hatuwezi kukubali kuona watanzania wakidhulumiwa namna hii,”
alisisitiza Waziri.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), akizungumza na wawekezaji mbalimbali katika sekta ya madini, waliowasilisha maombi ya kupatiwa leseni kwa ajili ya kuwekeza katika sekta husika.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akisaini leseni mbalimbali za wawekezaji katika sekta ya madini.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akikabidhi leseni ya uchimbaji wa kati wa madini ya ‘Marble’ iliyohamishwa kutoka kwa Salim Mohamed Salum (wa pili kutoka kushoto) kwenda kwa wawekezaji wa kampuni ya S & T Marble and Mining Limited (kulia). Wa kwanza kushoto ni Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...