Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza baada ya kupokea ripoti ya pili ya Kamati ya Wachumi na Wanasheria aliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza Mchanga wa Madini unaosafirishwa kwenda nje ya nchi, Ikulu jijini Dar es salaam leo. katika hotuba yake, Rais Dkt. Magufuli alisema "Mtanzania yoyote mwenye akili timamu ukisikia ripoti kama hii inatia uchungu sana, na ndio maana nashindwa hata niazie wapi" 

"Mwenyezi Mungu alituwekea rasilimali nyingi ili zitunufaishe Watanzania...madini tuliyonayo Watanzania ni madini ya kila aina na wala sio machache"

"Kampuni inafanya biashara ya trilions of money lakini hata haijasajiliwa nchini!! Mara ngapi tunawaumiza wamachinga wasio na leseni?".

"Wanasheria wapo tu, eti wanaogopa kushtakiwa. Yani mali yangu, mimi ndio nakulindia biashara yako, halafu uniibie, ukanishtaki, bado nikuache uchimbe?"

"Pamoja na mali hii yote, Mungu kutupendelea watanzania tumeendelea kuwa masikini, nina uhakika hata shetani aliko kule anatucheka kwa umasikini wetu ni wa kujitakia, lakini shetani huyu huyu tunayemlani inawezekana aliwatumia baadhi ya Watanzania wakati wakiwa ni viongozi"

"Wapo watanzania wenzetu waliopewa madaraka na Watanzania masikini kwa ajili ya kusimamia rasilimali zetu, lakini wamekuwa part ya kuwaibia Watanzania masikini"

"Kuna kampuni 6 ambazo wao hununua makinikia bila hata kuyaangalia kwa sababu wanajua kuna mali ndani."
"Mawaziri na wasaidizi wao kila siku wanaenda Ulaya lakini hawataki hata kukosea njia kwenda kuona hizo smelters".

 Katika ripoti hiyo iliyotolewa na Kamati imebaini kuwa Kampuni ya ACACIA MINE PLC haikusajiliwa nchini wala haina hati ya usajili na inafanya biashara ya madini nchini kinyume cha sheria, Pia Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Prof. Nehemia Osoro alisema kuwa Serikali imepoteza Kodi ya Mapato ya kiasi cha sh. trilioni 55 tangu mwaka 1998 hadi Machi 2017 katika usafirishaji wa makinikia, bilioni 94 Kodi ya Zuio ambayo Tanzania imepoteza tangu 1998 hadi Machi 2017 na kufanya Jumla ya thamani ya madini yaliyosafirishwa nje ya nchi kati ya 1998 hadi 2017 kwa Kiwango cha wastani ni trilioni 188.58.

TAARIFA KAMILI ITAKUJIA BAADAE KIDOGO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...