Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar
Mradi wa Kuimarisha huduma za
Afya Zanzibar (HIPZ) unatarajia kukusanya zaidi ya dola za Marekani
25,000 kwa ajili ya kusaidia huduma za afya katika Hospitali ya
Makunduchi na Kivunge ambazo wanazisaidia.
Fedha hizo zitapatikana kufuatia
kuandaa resi za baiskeli za kilomita 300 (Bike Ride 2017) katika mikoa
mitatu ya Unguja yatakayo dumu kwa muda wa siku sita kuanzia leo.
Akizungumza na waandishi wa
habari Hoteli ya Tembo, Mratibu wa resi hizo Dkt. Jon Rees kutoka
Uingereza amesema jumla ya wapanda baiskeli 25 kutoka Ulaya na Zanzibar
wanashiriki.
Amesema fedha hizo zitachangwa na
makampuni ya ndani na nje ya nchi na zitatumika kuimarisha huduma za
afya hasa afya ya mama na mtoto katika Hospitali za Kivunge na
Makunduchi.
Amesema Resi hizo ambazo ni mara
ya tatu kufanya Zanzibar zilianzia Mji Mkongwe kuzunguka maeneo mbali
mbali ya Mkoa Mjini Magharibi zitapitia Nungwi, Makunduchi, Kizimkazi na
zitrejea Mji Mkongwe.
Dkt. Ress amewataka wananchi wa Zanzibar kuwaunga mkono na kuwatia hamasa wapanda baiskeli hao hasa katika sehemu watakazopita.Akizindua resi hizo, Mkurugenzi
Kinga na Elimu ya Afya Dkt. Fadhil Abdalla Mohd amesema Mradi wa HIPZ
umeleta mafanikio makubwa katika ubunifu wake wa kutafuta fedha kwa
ajili ya huduma za afya kwa kuanzisha mbio hizo.
Amesema pamoja na kukusanya fedha
kwa ajili ya huduma za afya pia mbio hizo ni sehemu ya kuwashawishi
vijana kufanya mazoezi ambayo ni moja ya njia ya kujikinga na maradhi
yasiyoambukiza.
Dkt. Fadhil amesema wakati
serikali ipo katika mpango wa kuzipandisha daraja Hospitali ya
Makunduchi na Kivunge kuwa za Mkoa, fedha hizo zitatumika kuanzisha
majengo mapya na kuimarisha huduma za afya.
Mratibu wa resi za baskeli (Bike Ride 2017) Dkt. Jon Rees akizungumza na waandishi wa habari kuhusu dhamira ya mbio hizo Zanzibar ikiwa ni mara yake ya tatu.
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Abdalla Mohd akizungumza na washiriki wa resi za baskeli kabla ya kuanza rasmi zikiwa na lengo la kuimarisha huduma za afya Hospitali ya Kivunge na Makunduchi.
Picha ya pamoja ya washiriki wa Bike Ride 2017 wakifurahia mbio hizo kabla ya kuanza rasmi.
Washiriki wa resi za baskeli (Bike Ride 2017) wakikata maeneo ya viwanja vya Maisra kuendelea na safari yao itakayochukua sita sita.
Picha na Makame Mshenga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...