Mratibu wa Masoko wa
Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa akimkabidhi kompyuta mbili
Kaimu Mkurugenzi wa Mbulu, mkoani Manyara, Deogratias Kashasha.
Na Mwandishi Wetu, Mbulu
KWA miezi kadhaa sasa mvua
imeendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, hali inayoonyesha
kukidhi kiu ya watu wengi waliokuwa wakiiomba inyeshe katika maeneo yao.
Hata hivyo, licha ya mvua hiyo
kunyesha, lakini baadhi ya maeneo imekuwa na matokeo mabaya kutokana na kuezua
nyumba, kuharibu miundo mbinu muhimu ikiwamo ya barabara.
Matokeo hayo yameibua changamoto
mpya hususan za kufikika kwa urahisi katika maeneo hayo yanayoendelea kukumbwa
na mvua kubwa. Mbali na mvua hiyo kunyesha, hata hivyo uwajibikaji unaendelea
kufanyika kwa sekta na watu mbalimbali kuendelea na maisha yao ya kila siku ili
wakuze uchumi.
Zoezi la kutoa msaada wa kompyuta lilivyokuwa linaendelea katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Licha ya maeneo mengi
kukumbwa na mvua, lakini Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services
imeendelea na usambazaji wa kompyuta katika ofisi za serikali mikoani kama
ilivyozindua utaratibu huo mwishoni mwa mwaka jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...