Na Robert Hokororo


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack amefanya ziara wilayani Kishapu kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Katika ziara hiyo Telack alikagua mradi wa huduma ya maji kutoka Ziwa Victoria uliopo kata ya Maganzo na maendeleo ya ujenzi wa zahanati kata ya Shagihilu.

Mradi mwingine ni wa mjasiriamali wa kusindika alizeti na kukoboa nafaka za mpunga na mahindi ambao unatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.Kwenye kata ya Kishapu eneo la Mhunze alitembelea mradi mwingine wa ghala la kuhifadhi nafaka na mashine za kukoboa nafaka za mahindi na mpunga.

Katika ziara hiyo kiongozi huyo aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Albert Msovela na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa akiwemo Kamanda wa Polisi Mkoa was Shinyanga, Muliro Jumanne Muliro.

Alikaribishwa na mwenyeji wake, Mkuu wa wilaya, Nyabaganga Talaba, Katibu Tawala Wilaya, Shadrack Kangese, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga, Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya na wakuu wa idara katika halmashauri hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto) akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga wakati wa ziara yake wilayani humo. Wengine pichani kulia ni Kamanda wa Polisi mkoa huo, Muliro Jumanne Muliro.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akiangalia mashine za kukoboa na kusaga nafaka pamoja na kusindika alizeti kutoka mjasiriamali Mzee Nassoro alipokuwa kata ya Mwamamalasa.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kulia) akiwa na Katibu Tawala Mkoa, Albert Msovela (katikati) pamoja na Katibu Tawala Wilaya, Shadrack Kangese (kushoto) wakati wa ziara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...