Na Tiganya Vincent-RS-Tabora

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri amuagiza Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kushirikana na Kampuni zenye leseni ya uchimbaji madini ya dhahabu kuhakikisha wachimbaji wadogo wadogo na wafanyabiashara waliopo eneo la machimbo ya dhahabu ya Kitunda wanapatiwa vitambulisho kwa ajili ya kuimarisha usalama na utambuzi wao wakati wakifanya shughuli hiyo.

Bw. Mwanri alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na Watendaji wa Halmashauri ya Sikonge na viongozi wa Kampuni zote zilizopewa leseni ya uchimbaji madini ya dhahabu katika eneo la Kitunda.

Alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuwatambua wachimbaji wadogo wadogo na wafanyabiashara  wote walioajiriwa na wale waliojiajiri  ili kuepuka mgongano ambayo umekuwa ukijitokeza kwa baadhi ya wachimbaji wadogo wadogo kuvamia machimbo ya wenzao wanaposikia yana dhahabu na hivyo kusababisha mrundikano wa watu wengi katika shimo moja na kuhatarisha usalama wao.

Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza kuwa vitambulisho hivyo pia vitasaidia kuwatambua wachimbaji wadogo wadogo wa Kampuni moja na nyingine  ili kuepuka vurugu.

Alisema kuwa kabla ya zoezi hilo kufanyika ni vema uongozi wa Halmashauri na Kampuni zote uwe na taarifa sahihi za mhusika ikiwa ni pamoja na mahali alipozaliwa na uraia wake ili kuepuka kutoa ajira kwa wageni badala wachimbaji wadogo wadogo wa Kitanzania.

Bw. Mwanri alisema mtu asianze kazi za uchimbaji kabla ya kusajiliwa katika daftari kubwa na lile na mitaa ili Serikali ijue ni nani waliopo hapo na wanatoka wapi katika nchi hii ya Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...