Na Is-haka Omar, Zanzibar.  
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ ameshiriki katika mazishi ya watoto wanne waliofariki dunia  jana (juzi) baada ya kuingia kwenye gari iliyokuwa sehemu ya maegesho na likajifunga hali iliyopelekea watoto hao kukosa hewa na kufariki huko Kidongo Chekundu Unguja.   
Marehemu hao waliotambuliwa kwa majina ya Mwatma Mohamed Malawi (2), Haisam Mustafa(2), Munawar Ahmed Khamis (3) na Muslim Hamza bakar (2) wote wamezikwa leo katika maeneo tofauti ya Makaburi ya Mwanakwere na Kiembe samaki Mbuyu Mnene Unguja. 
Akizungumza mara baada ya maziko hayo Naibu Katibu huyo huko katika makaburi ya Mwanakwerekwe, alisema CCM imepokea kwa masikitiko na mshituko mkubwa taarifa ya vifo vya watoto hao na inatoa mkono wa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizopata msiba huo na kuwasihi waendelee kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki cha msiba huo.
Alisema watoto hao walitarajiwa kuwa ni miongoni mwa viongozi na wataalamu wa fani mbali mbali wa baadae hivyo msiba huo umeacha pengo kubwa  kwa familia na taifa kwa ujumla.
Aidha Dkt. Mabodi aliwataka wazazi na walezi nchini kuwa karibu na watoto wao kwa kuhakikisha mazingira yanayotumiwa na watoto kucheza yanakuwa katika hali ya usalama ili kuepuka athari zinazoweza kusababisha majeraha ama vifo kwa watoto wao.
 Maiti za watoto wanne waliofariki ndani ya gari huko Kidongochekundu  Zanzibar wakitolewa msikitini na kupelekwa katika makaburi ya Mwanakwerekwe kwa ajili ya mazishi.

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi' akishirikiana na waombolezaji wengine katika mazishi ya watoto hao.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi' akishirikiana na waombolezaji wengine katika mazishi ya watoto hao. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...