Zaidi ya kaya 700 za wananchi wa Kitongoji cha Irmorijo Kijiji cha Emairete Wilayani Monduli Mkoani Arusha, waliokuwa wanatumia maji ya kwenye bwana wanatarajia kunufaika na mradi wa kusafisha maji na kuchuja maji kuwa safi uliozinduliwa Kijiji hapo.

Awali, wananchi hao walikuwa wanatumia kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kupika, kufua, kuoga na kunywa maji hayo ya bwawa ambayo pia yalikuwa yanatumiwa na mifugo ya eneo hilo.

Mkurugenzi wa kampuni ya Smart Vision ya Korea, Seo Young Kim akizungumza jana kwenye uzinduzi wa mradi alisema lengo ni jamii ya eneo hilo kunufaika na maji safi na salama yanayochujwa kupitia ubunifu wao.

Kim alisema kwa kuanza kuwanufaisha wananchi wa eneo hilo, wanatarajia kugawa majiko rafiki ya mazingira 22 na mitambo ya kuchuja na kusafisha maji ya bwawa kuwa safi na salama 22 kwa kaya 22 zitakazowanufaisha zaidi ya watu 220.

Alisema Smart Vision kupitia uwekezaji wa Korea Trade-Investment Promotion Agency. (KOTRA) jamii ya eneo hilo itanufaika na na mradi huo wenye lengo la kuondokana na matumizi ya maji yasiyo safi wala salama ambayo yanasababisha magonjwa ya tumbo.

“Jamii ya eneo hili kupitia mchungaji wa kanisa la Enyorata Daniel Vengei, walileta maombi kwetu kuwa wanatatizo la maji, hospitali na shule, ndipo tukaona tuanze kutatua hili suala la maji ndipo tukaleta mitambo hii ya kuchuja na kusafisha maji,” alisema Kim. 
Mkurugenzi wa kampuni ya Smart Vision ya Korea, Seo Young Kim (kushoto) na Andrew Chung ambaye ni mbunifu wa mtambo wa kusafisha maji wakionyesha mtambo huo kwenye uzinduzi wake kwenye kitongoji cha Irmorijo Kijiji cha Emairete Wilayani Monduli Mkoani Arusha
Mkurugenzi wa kampuni ya Smart Vision ya Korea, Seo Young Kim (kushoto) na mchungaji wa kanisa la Enyora Daniel Vengei wakiwa kwenye uzinduzi wake katika kitongoji cha Irmorijo Kijiji cha Emairete Wilayani Monduli Mkoani Arusha.
Wananchi wa kitongoji cha Irmorijo Kijiji cha Emairete Wilayani Monduli Mkoani Arusha wakishuhudia uzinduzi wa mtambo wa kusafisha maji na kuyachuja uliofanywa na kampuni ya Korea ya Smart Vision.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...