Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na
Usalama na Mbunge wa Muheza, Mhe. Balozi Adadi Rajabu (kulia)
akizungumza pale ujumbe wa Wabunge kutoka Bunge la Canada ambao ni
Wajumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada
ulipotembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini
Dodoma, ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu katika utendaji wa kazi
baina ya Mabunge hayo. Ujumbe huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha
Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ambae pia ni Mbunge, Ndg.
Yasmin Ratansi (wa pili kushoto), kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Mabunge
ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ambae pia ni Mbunge, Ndg. Kerry
Diotte na wa pili kulia, ni Katibu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya
Madola Tawi la Canada Ndg. Remi Bourgault.
Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada
ambae pia ni Mbunge, Mhe. Yasmin Ratansi (wa pili kushoto) akizungumza
pale ujumbe wa Wabunge kutoka Bunge la Canada ambao ni Wajumbe wa Chama
cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ulipotembelea Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma, ukiwa na lengo la
kubadilishana uzoefu katika utendaji wa kazi baina ya Mabunge hayo,
kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na
Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Mhe. Dotto Biteko, anaefuta ni Mwenyekiti
wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na
Mbunge wa Muheza, Mhe. Balozi Adadi Rajabu , kushoto ni Mjumbe wa Chama
cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ambae pia ni Mbunge,
Mhe. Kerry Diotte na katikati ni Katibu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya
ya Madola Tawi la Canada Ndg. Remi Bourgault.
Ujumbe
wa Wabunge kutoka Bungela Canada ambao ni Wajumbe wa Chama cha Mabunge
ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada walipotembelea Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Mhe.Yasmin Ratansi (watatu kushoto),
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na
Usalama na Mbunge wa Muheza, Mhe. Balozi Adadi Rajabu (wa pili kushoto),
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbunge
wa Jimbo la Bukombe, Mhe. Dotto Biteko (wanne kushoto) na Katibu wa
Bunge, Dkt. Thomas Kashililah (wa tatu kulia). Ujumbe ukiwa na lengo la
kubadilishana uzoefu katika utendaji wa kazi baina ya Mabunge hayo.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...