Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anaondoka nchini leo kwenda Pretoria Africa ya Kusini ambako atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika utakaofanyika Pretoria, Afrika Kusini tarehe 19 na 20 Agosti, 2017. 

Mkutano huo utapokea na kujadili ajenda mbalimbali ikiwemo uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa SADC na Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama; Hali ya Michango mbalimbali ya Nchi Wanachama na Kupokea taarifa ya Mwenyekiti anayeondoka wa SADC Organ.  

Pia Mkutano utapokea taarifa ya Katibu Mtendaji wa SADC; Kupitia hali ya kiuchumi katika Kanda ya SADC; Kuwasilisha Kaulimbiu ya Mkutano wa SADC; Taarifa kuhusu Mfuko wa Maendeleo wa SADC; Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Viwanda; Kuwezesha Chuo cha Elimu ya Sayansi na Teknolojia; Maombi ya Serikali ya Comoro na Serikali ya Burundi kujiunga na SADC; Utekelezaji wa Mabadiliko ya Kitaasisi ya Umoja wa Afrika na Mkutano wa Mshikamano kati ya SADC na Saharawi ya Magharibi. 

Mkutano huo utatanguliwa na Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili ya SADC (SADC Double Troika Summit) tarehe 18 Agosti, 2017 ambao Tanzania itakabidhi nafasi ya  uenyekiti kwa mwenyekiti mpya. Double Troika inahusisha nchi wanachama sita ambao kwa sasa ni Swaziland, Tanzania, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji. Katika mkutano huo Mfalme Mswati III wa Swaziland atakuwa ndiye Mwenyekiti. Ajenda kuu katika Mkutano huu ni kupokea na kujadili taarifa kuhusu hali ya kisiasa, kiulinzi na kiusalama katika Kanda na hasa nchini DR Congo na Lesotho.

Makamu wa Rais amefuatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa AfrikaMashariki, Mhe. Balozi Dkt Augustine Mahiga, Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijange, Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Ashatu Kijaji na watendaji wengine waandamizi Serikalini

Makamu wa Rais na ujumbe wake anatarajia kurudi nchini Agosti 21, 2017.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
17/8/2017
 Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke ,Felex Jackson katika Uwanja wa Ndege wa Julias Nyerere Dar es salaam leo Agosti ,17/2017 akielekea Nchini  Pretoria Africa ya Kusini ambako atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika utakaofanyika Pretoria, Afrika Kusini tarehe 19 na 20 Agosti, 2017.
 Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Temeke ,Felex Jackson katika Uwanja wa Ndege wa Julias Nyerere Dar es salaam leo Agosti ,17/2017 akielekea Nchini  Pretoria Africa ya Kusini ambako atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika utakaofanyika Pretoria, Afrika Kusini tarehe 19 na 20 Agosti, 2017.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...