Na. Hassan Mabuye.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikishirikiana na Wizara ya Fedha, imesambaza maafisa wake katika halmashauri 169 kote nchini.

Maafisa hawa wanaotoa mafunzo katika vituo vyote vya makusanyo ya kodi ya ardhi na tozo nyingine kwa kutumia simu ya mkononi ili kuondoa kabisa mfumo wa zamani wa malipo.

Zaidi ya maafisa 170 kutoka makao makuu ya Wizara ya Ardhi, Wizara ya Fedha na kutoka kanda nane za ardhi wameanza kutoa elimu hiyo katika halmashauri na vituo vyote vya makusanyo ya kodi ya ardhi ili kurahisisha ulipaji kodi ya ardhi kwa wananchi kwa kutumia simu zao na kuondoa usumbufu.

Mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa njia ya simu ya mkononi ni mfumo wa kielektroniki wa Government electronic Payment Gateway (GePG) katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi ambao utamrahisishia mwananchi kulipia popote walipo kwa kutumia simu zao kwa urahisi zaidi.

Mwananchi yeyote anayemiliki kiwanja au shamba lililopimwa na kupatiwa hati, ataweza kutumia simu yake ya mkononi kujua kiasi cha kodi ya pango la ardhi anachodaiwa na kukulipa kwa kutumia simu yake ya mkononi.

Ili kujua unadaiwa kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi kwa kutumia simu ya mkononi bonyeza *152*00# au kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi yaani sms halafu unatuma kwenda namba 15200 na baada hapo unaweza kulipia kwa njia ya Mpesa, Tigo Pesa au kulipia tawi lolote la benki ya NMB na CRDB.
 Afisa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bwana Haruna Kiyungi akieleza jinsi ya kutumia Mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa njia ya simu ya mkononi/kielektroniki
 Afisa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi Bwana David Malisa (katikati) akitoa mafunzo kwa Maafisa kutoka Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi kanda ya Ziwa jinsi ya kutumia Mfumo wa GePG
 Afisa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Joines Mhalila akielekeza jinsi ya kutumia simu katika kufanya malipo ya kodi ya ardhi.

  Afisa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bwana Haruna Kiyungi akionesha kwa vitendo jinsi ya kutumia Mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa njia ya simu ya mkononi/kielektroniki.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...