WATOTO wanajengwa kwa kiakili  kwa kusoma vitu vinavyomuandaa katika kupenda shule katika ukuaji wa na kuleta matunda kwa taifa kutokana na msingi wa kusoma vitu mbalimbali.

Hayo ameyasema Afisa Mtendaji Mkuu wa Toto Magazine, Jacqueline Lesika wakati wa Tamasha la Kuogelea kwa wanafunzi wa Awali ya Shule ya  Shree Hindu Mandal amesema kampuni ya Toto Magazine  imeamua kudhamini tamasha hilo na kutoa zawadi ya jarada la watoto ili waweze kusoma.

Amesema kuwa jarida la watoto wanaweza kujifunza vitu ambavyo vitafanya watoto kupenda kusoma jarida hilo na kuacha kutumia muda wa kuangalia Luninga zenye katuni ambazo hazimjengei msingi wa elimu.

Jacqueline amesema kuwa wataendelea kushiriki matamasha mbalimbali yanayohusu watoto katika kuweza kuwapa elimu katika majarida ya watoto.

 Amesema kampuni ya Toto Magazine ni kampuni pekee ambayo imejikita kutoa elimu kwa watoto katika kuwajengea msingi wa elimu wa kupenda shule.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Toto Magazine, Jacqueline Lesika akimkabidhi cheti  na Jarirda la Toto kwa  Mwanafunzi wa awali katika shule ya Shree Hindu Mandal, Hussein Swedi kwa ushindi wa mashinadano ya kuogelea katika shule hiyo kwa udhamini wa Toto Magazin iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Toto Magazine, Jacqueline Lesika akimkabidhi cheti  na Tshirt ya Toto Magazine  Jarirda la Toto kwa  Mwanafunzi wa awali katika shule ya Shree Hindu Mandal, Rabil Faraji kwa ushindi wa mashinadano ya kuogelea katika shule hiyo kwa udhamini wa Toto Magazin iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Toto Magazine ,Jacqueline Lesika akizungumza na waandishi habari hawapo pichani juu udhamini wa Tamasha la Kuogelea kwa Wanafunzi wa Shule ya Awali ya Shree Hindu Mandal jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...