Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ametangaza kuwa hatashiriki kwenye uchaguzi mkuu ambao umepangwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu.
Bwana Odinga anasema anataka kufanyika uchaguzi mpya jinsi ilivyoamuliwa na mahakama ya juu.Uchaguzi huo wa tarehe 26 utakuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu, baada ya mahakama ya juu nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu.

Bw. Odinga anasema amejiondoa ili kuipa tume ya uchaguzi IEBC muda wa kutosha kufanya mabadiliko ambayo yatawezesha kufanyika uchaguzi kwa njia nzuri.Awali tume ya uchaguzi ilikuwa imemtangaza rais wa sasa Uhuru Kenyatta kuwa mshindi.Ilisema kuwa Bw. Kenyatta alishinda uchaguzi huo kwa kura milioni 1.4.Upinzani nchini Kenya awali ulikuwa umetangaza wazi kuwa ungeshiriki kwenye uchaguzi mkuu ikiwa mabadiliko yanayostahili yangefanyika.

Upinzani unaamini kuwa uchaguzi unastahili kufutwa baada ya Odinga kujiondoa, na kutoa muda wa kutosha kufanyika mabadiliko yanayostahili ili uchaguzi kufanyika kuambatana na sheria na katiba.

Serikali imekuwa ikisema kuwa uchaguzi utafanyika na rais kuapishwa.Bw. Odinga pia ametoa wito kwa watu kuandamana kesho Jumatano kwa kutumia kauli mbiu "hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi".
Mwezi Septemba mwendesha mashtaka mkuu nchini Kenya Keriako Tobiko, aliamrisha polisi na tume ya kupambana na ufisadi kuchunguza ikiwa wanachama wa tume ya uchaguzi walihusika na uhalifu wowote.
Alitaka wachunguzi kuchunguza madai kuwa maafisa wawili wakuu wa upinzani walikuwa wamedukua mitandao ya tume ya uchaguzi.
Baadhi ya Viongozi wa NASA walipokuwa wakizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema leo kuhusiana na kujiondoa kwao kwenye uchaguzi mkuu  wa marudio. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...