SHULE
mbili za manispaa ya Kinondoni shule ya Kigogo na Mkwawa zaadhimisha siku ya unawaji mikono
ambayo hufanyika kila mwaka Oktoba 13 ikiwa na kaulimbiu ya mikono safi
kwa manufaa ya sasa na ya baadae.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta amesema kuwa kila mtoto
anatakiwa kunawa mikono kabla na baada ya kula pamoja na watokapo
masalani ili kuepukana na maradhi ya kipindupindi na maradhi yaletwayo
kwa kula uchafu.
Amesema
kuwa siku hii ni muhimu hasa kwa watoto wanaokurupuka kumegeana vyakula
au vitafunwa wawapo shuleni bila ya kunawa mikono yao na bila ya kujua
ni nini madhara ya kula bila kunawa.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta akizungumza wakati wa
kuadhimisha siku ya kunawa mikono iliyofanyika katika shule ya Msingi
Mabibo na shule ya Msingi Mkwawa jijini Dar es Salaam leo.
Pia
amewaasa wanafunzi wa shule za msingi Kigogo pamoja na Mkwawa kunawa
mikono mikono kila wanapotaka kula na baada ya kula pia marabaada ya
kutoka maeneo ambayo wanashika uchafu.
Wanafunzi
wa shule ya Msingi Kigogo na shule ya msingi Mkwawa wakiwa katika siku
ya kunawa mikono iliyoadhimishwa shuleni hapo kwaajili kuelewa manufaa
ya kunawa mikono kabla ya kula, baada baada ya kula, na baada ya
kutoka msalani kwaajili ya kujikinga na maradhi yanayoletwa na kuto
kunawa mikono.
Mwanafunz
wa chuo Kikuu cha Muhimbili Kerobe TEHSA akiwafundisha watoto jinsi ya
kunawa mikono kwa kutumia kibuyu chirizi ambacho ni rahisi zaidi kuliko
kuchota maji kwa kutumia kikombe ambayo ni kwaajili ya kunawa mikono
kabla na baada ya kula na wakati watokapo msalani hii ikiwa ni siku ya
unawaji Mikono iliyoambatana na kauli mbiu ya Mikono safi kwa manufaa ya
sasa na yabaadae.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...