Na
Hamza Temba – WMU
..........................................................
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga ameuagiza uongozi wa Wakala wa Huduma
za Misitu Tanzania (TFS) kubuni utaratibu mpya ikiwemo kuanzishwa kwa chombo kitakachosimamia
upangaji wa madaraja ya ubora wa mbao zinazozalishwa hapa nchini ziweze kukidhi
viwango vya mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.
Ametoa agizo hilo jana
kwenye kikao cha majumuisho na watumishi wa Shamba la Miti la Serikali la
Kiwira ambalo linasimamiwa na wakala huyo wakati anahitimisha ziara yake ya
kikazi ya siku moja katika Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.
“Kuna changamoto kubwa
kwenye soko la mbao, kwa kiwango kikubwa mbao zetu nyingi tunaziuza hapa
nchini, Lazima tufike mahali hizi mbao tuwe tunaziexport (uza nje) kwa kiwango
kikubwa. Lakini ili tufikie malengo hayo mbao zetu lazima ziwe kwenye kiwango
kinachokubaliwa.
“Mbao zinazokuwepo
kwenye soko letu la ndani huwezi kuzitenganisha kwamba hizi ni za TFS au za mwananchi wa kawaida, nyingine zina ubora nyingine
hazina, agizo langu kwenu kaeni chini kama watendaji tuje na utaratibu
utakaotuwezesha kuzipanga kwenye madaraja, daraja la kwanza, la pili, la tatu
au la nne ili mnunuzi ajue ananunua mbao ya ubora wa aina gani,” alisema
Hasunga.
Alisema amepata
taarifa kuwa baadhi ya wananchi wanavuna miti ambayo haijakomaa jambo ambalo
linaathiri ubora wa mbao kwenye soko kwa kutokidhi mahitaji ya wateja, hivyo akaagiza
Wakala huyo kubuni mbinu mpya za kuwalinda wateja ikiwemo kuanzishwa kwa chombo
maalum cha udhibiti wa ubora wake.
"Kwa maeneo
mengine tuna TBS, kwenye chakuka tuna TFDA, kwenye mbao je? Nani
anaregulate?(dhibiti), ni lazima tufike mahali tuwe na mdhibiti atakayetusaidia
kuhakikisha kwamba ubora unakuwepo,” alisema Hasunga.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto) akizungumza na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja (wa pili kushoto) alipofika ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo akiongozana na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza (wa pili kulia) kwa ajili ya kujitambulisha wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani humo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akimsikiliza Meneja wa Shamba la Miti Kiwira, William Dafa wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi katika shamba hilo jana katika Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...