Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakanusha taarifa inayosambaa katika Mitandao ya Kijamii kuhusu Taasisi ya Kiraia ijulikanayo kama Samia Habari Suluhu. 

Taasisi hiyo inajitambulisha  kuwa inatoa mikopo ya fedha taslim, pikipiki na bajaji kwa wanawake wajasiriamali kwa masharti ya kuweka dhamana ya fedha taslimu shilingi laki mbili. Ofisi inapenda kuujulisha umma kuwa taarifa hizo ni za uongo na uzushi na zina lengo la kuupotosha umma wa Watanzania.

Makamu wa Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, hamiliki taasisi yoyote ya aina hiyo na hahusiki kwa namna yoyote na kazi za taasisi hiyo na wala haitambui taasisi hiyo.

Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka Wananchi kuzipuuza taarifa hizo zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwani zinalenga kuleta taharuki na kupotosha Umma wa Watanzania.

Imetolewa na:
Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ikulu- Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...