NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewataka wananchi kushirikiana na serikali katika kuvitangaza vivutio vya utalii ili kuongeza pato la taifa.

Amezungumza hayo leo wakati wa mahafali ya 15 ya Chuo cha Taifa cha Utalii yaliyofanyika kwa kuunganisha matawi ya chuo hicho nchini.Hasunga amewatunikia wanafunzi 129 wakiweza kutunukiwa shahada na astashahada katika fani za upishi, usafi wa vyumba, uhudumu wa chakula na usafirishaji wa watalii.

Katika mahafali hayo, Niabu Waziri Hasunga amewataka wananchi smabamba na wadau mbalimbali wa utalii kushirikiana na serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kuutangaza utalii kwani ni sekta mtambuka.

Kwa sasa seriikali mfumo wa kuwasajili wanafunzi wote walisomea masuala ya utalii ili kuweza kufahamu idadi yao ukamili na pia kuweza kuwafahamu wale ambao wapo katika sekta ya utalii wakiwa hawajapitia katika mafunzo yoyote.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akifungua pamoja na kuzungumza na wahitimu na wageni waalikwa wakati mahafali ya kumi na tano(15) ya Chuo cha Taifa cha Utalii yaliyofanyika leo katika kampasi ya Bustanini jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Taifa cha Utalii, Bernadetha Ndunguru akizungumza kuhusu namna bodi inavyofanya kazi yake ili kufanikisha Chuo hicho kinafikia malengo waliyojiwekea wakati wa mahafali ya kumi na tano(15) ya Chuo cha Taifa cha Utalii yaliyofanyika leo katika kampasi ya Bustanini jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii. Dkt. Shogo Muzola akizungumza kuhusu mafanikio na hali ya elimu katika chuo hicho wakati wa mahafali ya kumi na tano(15) ya Chuo cha Taifa cha Utalii yaliyofanyika leo katika kampasi ya Bustanini jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiwakabidhi baadhi ya wahitimu wa vyeti pamoja na zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri wakati wa masomo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...