Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo ametoa wiki sita kwa Mkandarasi wa mradi wa maji Kivindo Wilayani Muheza kukamilisha mradi huo na uanze kutoa huduma kwa wananchi.

Waziri Jafo ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake Wilayani Muheza ambapo alikagua miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo.

Alisema Mradi huo kwas asa umefikia asilimia 90 ya utekelezaji wake na Mkandarasi umeahidi hapa mbele ya wananchi kwamba utaukamilisha ndani ya muda niliokupa ambao ni wiki sita kuanzia hivi sasa.

“Sitegemei kuskia sababu zozote zitakazofanya mradi huu usikamilike ndani ya wiki sita ni mategemeo yangu wananchi wataanza kufaidi matunda ya mradi huu baada ya muda mfupi tu kuanzia sasa, Mkandarasi fanya kazi yako” Alisema Jafo.

Katika ziara hiyo Waziri Jafo amefanikiwa kutembelea Miradi ya afya na elimu katika kituo cha afya Mkuzi na Ubwari pamoja na kutembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Kilulu. 

Waziri Jafo amewapongeza wadau mbalimbali wanaoshirikiana na Serikali katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika Maeneo ya Umma. Hususan ni Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMRI) kwa kutoa mifuko 50 ya Saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa miundombinu katika kituo cha Afya Ubwari.

Halkadhalika Waziri Jafo ametoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kuendelea kushirikiana na Serikali katika kufanikisha ajenda ya maendeleo kwa wananchi.
Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akiwa katika kituo cha Afya Ubwari wakati wa ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.
Waziri Jafo akiwa katika Ukaguzi wa Miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Muheza.
Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI akiwa na baadhi ya viongozi katika Halmashauri ya Wilaya ya Muheza.
Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI akiwa na baadhi ya vijana waoashiriki kuchimba mitaro ya mradi wa Maji Kivindo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...