Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia-TBL, Bw. Roberto Jarrin ambaye ameahidi kuwa kampuni yake itajenga kiwanda kikubwa cha bia kitakachogharibu takriban dola milioni 100 za Marekani, mkoani Dodoma.

Jarrin ameeleza kuwa hatua hiyo inalengo la kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.Amesema kuwa mafanikio makubwa ambayo kampuni yake imeyapata hapa nchini hasa baada ya kubadilisha ujazo wa kinywaji chake kimoja umeifanya Kampuni yake ifikirie kuongeza uzalishaji kwa kuongeza kiwanda kingine mkoani humo.

Bw. Jarrin amebainisha kuwa upanuaji wa huduma zake nchini utakwenda sambamba na kuendeleza kilimo cha mazao yanayotumika kutengenezea vinywaji hususan shayiri ama ngano hatua ambayo itawanufaisha wakulima nchini.Akizungumza katika kikao hicho, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango ameuelezea mpango huo wa TBL kwamba utachochea ukuaji wa uchumi na ajira kwa wananchi.

“Tunataka kujenga Tanzania ya viwanda, na TBL ni kiwanda ambacho kitanipa ajira kwa Watanzania, kitanipa kipato zaidi, lakini pia nataka Dodoma iwe kitovu kingine cha uchumi kwa kutupatia mapato kama ilivyo Dar es Salaam inayochangia zaidi ya asilimia 80 ya mapato ya Serikali” alisema Dkt. Mpango.Ameunda timu ya wataalamu itakayopitia na kuchambua masuala mbalimbali ya kikodi na kisera yaliyowasilishwa na kampuni hiyo ili yafanyiwekazi haraka kwa manufaa ya pande hizo mbili.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Roberto Jarrin, alipokuwa anamueleza nia ya Kampuni hiyo kuwekeza mkoani Dodoma, alipomtembelea Dkt. Mpango ofisini kwake mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akimsikiliza Kamishna Msaidizi-Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Shogholo Msangi akifafanua jambo wakati Waziri Mpango, alipokutana na kufaya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Bw. Roberto Jarrin, uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Roberto Jarrin, akifafanua jambo wakati wa mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mijini Dodoma.


Watumishi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakichukua kumbukumbu wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Roberto Jarrin (hawapo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...