NA TIGANYA VINCENT

WAKULIMA wa Pamba mkoani Tabora wametakiwa kudiriki kuuza  mazao yao kwa Kampuni ambazo hazikuwakopesha mbegu na viuawadudu ili kuzidisha imani kwa waliosaidia kuwapa mbegu kwa utaratibu wa kulipa baada ya mavuno.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati alipokuwa akikagua mashamba mbalimbali ya wakulima wa pamba Wilayani Igunga ili kujionea maendeleo ya kilimo cha zao hilo.

Alisema kuwa uaminifu ambao watauonyesha mara baada ya kuvuna na kuuza pamba katika Kampuni zilizowakopesha mbegu na viuawadudu itawajenga Imani kwa wakopeshaji kuangalia uwezekano wa kupanua wigo wa kuwasaidia wakulima ,hata ikiwezekana kuwakopesha mbolea kwenye kilimo msimu mwingine.

 “Nawaombeni wakulima wangu wazuri mjitahidi kuwa waaminifu kwa Kampuni zilizowakopesha mbegu na viuawadudu …kwani uaminifu wenu utawasaidia viongozi wenu kukaa meza moja na Kampuni  ili kuziomba ikiwezekana katika kilimo cha mwakani wawakopesha na mbolea” alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

“Lakini mtakapovuna pamba yenu na kuitorosha kwa kubadilisha majina wakati wa uuzaji inaweza kusababisha Kampuni zikakataa kuwasaidia tena” alisema Mwanri.

Alisema kuwa mkulima atakayekamatwa kutaka kutorosha pamba ili kukwepa gharama za mbegu na viuawadudu atachukuliwa hatua ili ije fundisho kwa wakulima wengine wenye tabia hiyo. Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwaagiza Maofisa Ugani washirikiane na Maofisa Watendaji wa kuanzia Kata hadi Kata kuhakikisha wanaorodhesha wakulima wote waliokopeshwa mbegu za pamba ikiwa ni pamoja na kiwango walichochukua na eneo walilolima ili kuwa na uhakika.

Mwanri alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kuepusha udanganyifu na ukwepaji unaoweza kufanywa na baadhi ya wakulima wachache ambao sio waaminifu kwa kudanganya majina au kutumia jina tofauti na lile ambalo hatalitumia wakati wa mauzo. Alisema kuwa vitendo vya aina hiyo ndivyo vilisababisha baadhi ya vyama vya msingi kufa kwa sababu ya kuwa na wakulima wenye tabia ya kutaka kukopesha lakini hawapendi kulipa mkopo.

Mwanri alisema kuwa ni vema viongozi wakawa makini wanakamilisha haraka kabla hata wakulima hawajaanza kuvuna pamba yao.

Naye Mkaguzi wa wa Pamba wilayani Igunga George Kihimbi alisema kuwa tayari wameshaanza kukusanya takwimu za wakulima wote na ukubwa mashamba waliyolima ili kupata usahihi wa pamba ambayo inatarajiwa kuvuna.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...