Na David John
WAKULIMA wa zao la Karafuu Kata ya Kigongoi Mashariki wilayani Mkinga mkoa wa Tanga wameiomba Serikali kuwapatia soko la uhakika la zao hilo kwani kuzalisha wanazalisha lakini hawana soko.

Wamesema kuwa katika kata yao hiyo wananchi wake wanalima kwa wingi zao la karafuu lakini pamoja na jitihada hizo za kulima lakini wanakosa soko la uhakika nakuwavunja moyo wa kuendelea kulima zao hilo.

Akizungumza kwaniaba ya wananchi wa kijiji cha Hemsambia Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho Stephen Komba alisema kuwa wananchi wake wanalima kwa wingi zao la karafuu lakini tatizo ni soko.

Alisema kuwa anaiomba serikali kupitia wizara inayohusika kufika kijiji hapo ili kujionea mwenyewe hali ilivyo na kuona namna ya kuwasaidia hususani kupatikana kwa soko la uhakika.

Mbali na changamoto hiyo ya soko la kukosekana kwa soko la karafuu pia kuna tatizo kubwa la miundombinu ya barabara na kwamba hata soko likiwepo tatizo barabara.

"Tunamuomba waziri wa viwanda biashara na uwekezaji Charles Mwijage pamoja na Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mnyaa Mbarawa kufika eneo hilo kujionea miundombinu ya barabara."alisema Pia alisema kuwa Wilaya ya mkinga inatatizo kubwa hususani kwenye miundombinu ya barabara pamoja na masoko ya mazao ya wakulima wao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...