Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Serikali kwa kushirikiana na wadau inaendeleza juhudi za kupambana na ukatili wa kijinsia, ndoa na mimba za utotoni kwa kuwawezesha walimu wa shule za sekondari kwa kuwapa mbinu za kupambana na vitendo hivyo  katika maeneo yao.

Hayo yamesemwa mjini Dodoma na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Bi. Magreth Mussai alipokuwa akifunga mafunzo ya kupambana na ukatili wa kijinsia, ndoa na mimba za utotoni yaliyoandaliwa na walimu wenyewe kwa kushirikiana na Serikali na shirika la Femina.

Bi Magreth Mussai amesema kuwa katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia Serikali ilizindua Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Jinsia wa mwaka 2017/2018 hadi  mwaka 2020/2021.

Ameongeza kuwa katika kutekeleza Mpango mkakati wa Kupambana na ukatili wa kijinsia Wizara ilianzisha  kampeni ya kutokomeza ndoa na mimba za utotoni iliyozinduliwa na Wizara hivi karibuni Mkoani Mara inayosema: “Mimi ni Msichana Najitambua na Elimu ndio Mpango Mzima”
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Bi. Magreth Mussai  akieleza namna Serikali inavyoshirikiana na wadau na wananchi kupambana  na Ukatili wa kijinsia katika siku ya mwisho ya mafunzo ya kuwajengea ulewa walimu walezi wa shule za Sekondari Tanzania katika kupambana ukatili hususan ukeketaji, ndoa na mimba za utotoni kwenye mafunzo yaliyofanyika mkoani Dodoma.
 Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Familia Bi. Rose Minja akieleza jinsi Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinisa,Wazee na Watoto ilivyojipanga kutokomeza Ukatili wa kijinsia katika siku ya mwisho ya mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu walezi wa shule za Sekondari nchini hususan kuzuia ukeketaji, ndoa na mimba za utotoni kwenye mafunzo yaliyofanyika mkoani Dodoma.
 Mwakilishi wa Benki ya NMB PLC Bw. Rodgers Malangu  akieleza jinsia Benki hiyo inavyowezesha wazazi kuwekeza kwa watoto kwa lengo la kuwapa malezi na kuwafundisha utamaduni wa kuweka akiba kwa manufaa ya matunzo ya watoto wa Taifa hili katika siku ya mwisho ya mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu walezi wa shule za Sekondari Tanzania kupambana na ukatili wa kijinsia, ndoa na mimba za utotoni yaliyofanyika mkoani Dodoma.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Bi. Magreth Mussai akiwa katika picha ya pamoja na walimu walezi wa shule za sekondari mara baada ya kumaliza mafunzo ya kuwajengea uwezo kupambana na ukatili wa kijinsia, ndoa na mimba za utotoni yaliyofanyika mkoani Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...