Serikali ya Marekani kwa kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), imezindua mradi wa kuimarisha asasi za kiraia na vyombo vya habari uitwao Boresha Habari Katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 

Ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360, mradi wa Boresha Habari utashirikiana na wabia wa Kitanzania, ikiwa ni pamoja na  Baraza la Habari Tanzania, Tanzania Bora Initiative, na Jamii Media,ili kuboresha weledi miongoni mwa waandishi wa habari na kusaidia kuweka mazingira yaliyo wazi kwa vyombo vya habari. Shabaha kuu ya jitihada hizi itakuwa ni kushirikisha na kujenga uwezo wa wanawake na vijana ili kuinua sauti, usemi na masuala yao katika nyanja mbalimbali za jamii wakiwa ni wazalishaji na watumiaji wa habari. 

“Serikali ya Marekani imedhamiria kwa dhati kusaidia kuinua ujuzi na weledi wa vyombo vya habari na asasi zisizo za kiserikali za Kitanzania – hususan katika kuwawezesha wanawake na vijana – kupaza sauti zao na kueleza dukuduku zao kwa ufanisi,” alisema Mkurugenzi Mkazi wa USAID Andy Karas Wakati wa hafla hii. 

Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, mradi wa Boresha Habari unalenga kufanya kazi na wadau wa vyombo vya habari katika mikoa ya Dar es Salaam, Zanzibar, Iringa, Mbeya, Morogoro, Arusha, Manyara, Dodoma, Tanga, Mtwara, Mwanza na Kigoma. Aidha, mradi wa Boresha Habari utatoa mafunzo na msaada wa kitaalamu kwa vyombo vya habari vya humu nchini ukivisaidia kuanza kutumia teknolojia za kidijitali na kuimarisha uwezo wao wa kiusimamizi na kifedha. 

Hali kadhalika, mradi huu utatoa mafunzo kwa asasi za kiraia ili ziweze kushirikiana vyema na vyombo vya habari katika kusukuma mbele jitihada zao. Kwa kuzingatia umuhimu wa redio za jamii kama vyanzo maarufu vya habari za maeneo husika, mradi wa Boresha Habari utafanya kazi na vituo mbalimbali vya redio nchini kote ili kuboresha uwezo wao wa kitaalamu na uendelevu katika masuala ya kifedha. 

Executive Director of Tanzania Bora Initiative Abella Bateyunga (left) addressing participants during the launching of a civil society and media strengthening Boresha Habari project in Dar es Salaam yesterday. The 5 year USAID funded project will be coordinated by local organizations Internews and FHI 360 and implemented by a number of Tanzanian partners including Tanzania Bora Initiative, aims at enhancing professionalism amongst Tanzanian media and civil society with a particular focus of empowering women and youth – to raise their voices and concerns effectively as both producers and consumers of information. 
USAID Mission Director Andy Karas (right) congratulates Media and Communication Director of InterNews Wenceslaus Mushi after the launching of a civil society and media strengthening Boresha Habari project in Dar es Salaam yesterday. Looking on is the Executive Secretary of the Media Council of Tanzania Kajubi Mukajanga (center). The 5 year USAID funded project to be coordinated by local organizations Internews and FHI 360 and implemented by a number of Tanzanian partners including: the Media Council of Tanzania, Tanzania Bora Initiative, and Jamii Media aims at enhancing professionalism amongst Tanzanian media and civil society with a particular focus of empowering women and youth – to raise their voices and concerns effectively as both producers and consumers of information.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...