Na Joel Maduka, Chato
Kukamilika kwa ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndege wilayani Chato mkoani Geita unatarajia kuwavutia watalii wengi kutembelea kivutio cha hifadhi ya Taifa cha Rubondo Kilichopo mkoani humo .
Ujenzi wa uwanja huo umeanza rasmi mwezi wa Septemba mwaka jana na unatarajia kukamilika Juni mwaka huu.Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini (TANAPA), Jenerali Mstaafu George Waitara wakati alipotembelea uwanja huo pamoja na wajumbe wa bodi hiyo na baadhi ya watendaji kwa nia ya kujionea maendeleo ya ujenzi huo ambao umeelezwa kukamilika kwa asilimia 65.
“ Kiukweli niseme kazi kubwa sana ambayo imefanyika ya ujenzi wa uwanja huu utakuwa na faida kubwa sana kwaajili ya mambo ya utalii na mambo mengine kama ya biashara na suala jingine kubwa ni kuibua vivutio vingine tupate watalii wengi zaidi , tunatarajia utakapokamilika utaleta manufaa sana katika sekta mbali mbali zikiwemo za utalii na biashara mkoani Geita na mikoa ya jirani,”alisema Waitara.

Kwa upande wake, Mhandisi wa ujenzi wa uwanja huo,Makuye Muhinga,Alisema uwanja huo wenye barabara ya kutua ndege (run a way ) yenye urefu wa Mita 300 upo kwenye hatua nzuri na kwamba wanatarajia kukamilisha mwaka huu ujenzi wa uwanja.
Mwenyekiti wa wa Bodi ya Shirika la kuhifadhi Wanyamapori Tanzania (TANAPA), Jenerali Mstaafu,George Waitara akizungumza na Mhandisi wa ujenzi wa uwanja huo,Makuye Muhinga juu ya mikakati ambayo inaendelea ya ujenzi wa uwanja wa ndege Wilayani Chato mkoani Geita,wakati walipoutembelea. 
Barabara ya kutua ndege (run away) yenye urefu wa Mita 300 ambayo kwa sasa hipo kwenye hatua nzuri za mwisho kukamilika. 
Baadhi ya watendaji na wajumbe wa Bodi ya TANAPA wakikagua ujenzi wa mradi wa uwanja wa Ndege Wilayani Chato Mkoani Geita. 
Mwenyekiti wa bodi ya hifadhi za Taifa nchini (TANAPA), Jenerali Mstaafu,George Waitara akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Chato (Katikati) Shaaban Ntarambe pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi ,Robert Gabriel Luhumbi wakati walipofika na kujionea ujenzi wa uwanja wa ndege ambao unajengwa Wilaya ya Chato unavyokwenda kwa kasi. 
Mhandisi wa ujenzi wa uwanja huo,Makuye Muhinga akizungumza na Mwenyekiti wa bodi ya hifadhi za Taifa nchini (TANAPA), Jenerali Mstaafu,George Waitara pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Gabriel,Juu ya hatua ambazo wamezifikia hadi sasa za ujenzi wa uwanja wa Ndege. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...