Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeanza majaribio ya utumiaji wa teknolojia ya kisasa katika Idara ya Radiolojia ili kuharakisha utoaji wa majibu ya wagonjwa ambao wanafika katika idara hiyo kwa ajili ya kupima vipimo mbalimbali ikiwemo MRI, CT-Scan, Utra Sound pamoja na X-ray.

 Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu maboresho ya utoaji wa huduma katika hospitali hiyo , Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Profesa Lawrence Museru amesema kwa muda mrefu kumekua na changamoto ya utoaji wa majibu kwa wagonjwa kutokana na ripoti ya mgonjwa kupitia hatua kadhaa.
 Amefafanua kuwa teknolojia hiyo ambayo imewezeshwa na Chuo Kikuu cha Yale cha nchini Marekani itawawezesha wataalam kutoa majibu kwa wakati na haraka sanjari na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi hivyo kwenda kwenye ngazi za juu zaidi za huduma ya Raiolojia . 
 “Lengo letu ni kufanya majibu yatoke haraka na kuondokana na changamoto ya Daktari kutumia muda mrefu kuandika ripoti ya mgonjwa , kwani teknolojia hii ya kisasa inaondoa hatua karibu tatu ambazo zilimlazimu Daktari kuzipitia na hivyo mgonjwa kusubiri majibu kwa siku mbili hadi tatu hivyo kuanza kutumia mfumo huu ni hatua nzuri kwa hospitali na kwa wagonjwa, pia teknolojia hii itakapofanikiwa tutaipeleka pia katika Maabara yetu’’. Amesema Profesa Museru. 
 Akielezea kuhusu teknolojia hiyo Profesa Frank Minja ambaye ni mtaalam wa Radiolojia kutoka Chuo Kikuu cha Yale , amesema mfumo huo unatafsiri kwa sauti majibu ya mgonjwa , huku ukichapa moja kwa moja majibu hayo na kisha kumfikia Daktari wakati huohuo. 
 “Mfumo huu unasaidia sana kutoa majibu kwa wakati, kuongeza tija katika utendaji kazi na hutumika sana nchini Marekani , mfumo huu unatumia vipaza sauti , na unahitaji Kompyuta yenye nguvu hivyo tumejikita zaidi katika kuongeza kumbukumbu kwenye Kompyuta zetu na ndio maana tumekuja na mtaalam wa IT ambaye anasaidia katika mfumo huu lakini pia anatoa elimu kwa wataala wa MNH ’’ amefafanua Profesa Minja. 
 Hospitali ya Taifa Muhimbili katika Idara ya Radiolojia kwa siku imekuwa ikihudumia wagonjwa zaidi ya 200, asilimia 20 hupima kipimo cha MRI, Asilimia 25 CT-Scan, asilimia 30 Plain X-Ray, asilimia 23 Utra Sound na asilimia 2 vipimo vingine.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital i ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na waandishi wa habari baada kupokea msaada wa teknolojia ya kurekodi majibu kwa wagonjwa. Teknolojia hiyo itasaidia wagonjwa kupata majibu kwa wakati kwani hakutakuwa na haja ya wataalamu kuandika majibu na badala yake itarekodi moja kwa moja.  Kulia ni Bwana Tarek  El- Shayal kutoka Taasisi ya Afya na Elimu ya nchini Marekani ambaye amewezesha kupatikana kwa teknolojia hiyo. Kushoto ni Mtaalamu wa Radiolojia, Profesa Frank Minja kutoka Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani.
 Baadhi ya wataalamu wa radiolojia kutoka Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani wakiwa kwenye mkutano huo. Wengine ni waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital i ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akimkabidhi zawadhi ya diary Bwana Tarek  El- Shayal kutoka Taasisi ya Afya na Elimu ya nchini Marekani.
Mtaalamu wa Radiolojia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Frederick Lyimo akiwaeleza waandishi wa habari jinsi teknolojia hiyo inavyofanya kazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...