JESHI la Polisi mkoani Mwanza kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) mkoani hapa imemkamata Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Bw. Anthony Bahebe.

Pia Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bw. Alphonce Sebukoto naye amekamatwa na Jeshi hilo. 

Viongozi wote hao wanakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na ubadhilifu wa fedha za umma. Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema kukamatwa kwa viongozi hao kunatokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.

Kamanda Msangi alisema, Bw. Sebukoto alikamatwa Februari 19, 2017 na Bw. Bahebe amekamatwa leo na wote wanaendelea kuhojiwa na Polisi kwa kushirikiana na TAKUKURU.Naye Kamanda wa TAKUKURU wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Ernest Makale alisema Bw. Sebukoto aliidhinisha malipo ya sh.milioni 278 zilipwe katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. Bahebe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...