Jana 16/02/2018 baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe, walifika ofisi za Tume ya Taifa kuwasilisha malalamiko yao kadhaa ambayo walikuwa wanahitaji ufafanuzi kutoka NEC kuhusu uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam. 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya kupitia hoja za Chadema, inapenda kutoa ufafanuzi wa hoja hizo: 

Hoja ya kwanza, kwamba, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Uchaguzi la Kinondoni amekaa kuwaapisha mawakala wa ziada wa upigaji kura kutoka CHADEMA ambao ni asilimi kumi na tano (%15) ya Mwakala wote wanaohitajika kwenye vituo 613, na kuwa utaratibu huu umekuwa unatumiwa katika Chaguzi zilizopita. 

Ufafanuzi, kwa mujibu wa kifungu cha 57(1)(2) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, kila Chama cha Siasa kilichopata ridhaa ya kuweka wagombea, kinaweza kuteua wakala mmoja wa upigaji kura kwa kila kituo ndani ya jimbo. 

Aidha, Kanuni ya 48(2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za mwaka 2015 inakitaka kila Chama cha Siasa kinachoshiriki katika Uchaguzi siyo zaidi ya siku saba (7) kabla ya siku ya Kupiga Kura kiwe kimewasilisha kwa maandishi kwa Msimamizi wa Uchaguzi majina ya Mawakala, anwani zao na vituo walivyowapangia. 

Vilevile, kifungu cha 57(3) cha Sheria tajwa, kimeweka utaratibu na mazingira ambayo wa Chama kilichosimamisha Mgombea kuweka wakala mbadala wa upigaji kura. 

Tunashauri CHADEMA kuzingatia matakwa ya kifungu cha 57(3) cha Sheria husika pale patakapohitajika uwepo wa mawakala mbadala. 

Hoja ya pili, kwamba, Msimamizi wa Uchaguzi amekataa kuwaruhusu na Viongozi wa CHADEMA kuwa Mawakala wa upigaji kura, kwa maana hiyo atakichagulia chama mawakala wa upigaji kura, na kwamba, orodha ya viongozi hao watambuliwe na kuapishwa kuwa Mawakala wa upigaji kura. 

Ufafanuzi, kifungu cha 57(1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 kikisomwa pamoja na Kanuni ya 48(2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za mwaka 2015 vimeweka utaratibu wa muda wa kuwasilisha orodha ya mawakala na muda wa kuwaapisha kuelekea siku ya Uchaguzi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...