Jeshi la Polisi nchini kupitia kamisheni yake ya Polisi Jamii limetoa elimu kwa wananchi katika mkoa wa Lindi Wilaya ya Ruangawa Kata ya Nkowe,  Juu ya Matumizi salama ya mitandao mbalimbali ya Kijamii ili kuepuka kutokea kwa uhalifu wa aina mbalimbali.
Imeelezwa kuwa makosa ya kimtandao hufanywa na watu ambao tayari wana uelewa  mkubwa kuhusiana na  na matumizi ya teknolojia  na kisha kwenda kuwarubuni watu wenye uelewa mdogo kuhusiana na mitandao hiyo.
Hayo yamesemwa na Inspketa  wa  Polisi Issa Asali   wakati akizungumzana wananchi wa kata ya Nkowe wilayani Ruangwa  kwa lengo la kupunguza vitendo vya kiuhalifu  ambavyo kwa kiasi kikubwa vimekuwa vikitokea  nchini .
Katika ziara hiyo iliyoongozwa na Mkuu wa Kitengo hicho cha Polisi Jamii Naibu Kamishina wa Polisi DCP Ahmada.A. Khamis, Polisi  iliambatana na Maafisa wa  CRDB Bank kutoka Makao Makuu Dar es salaam,  ambapo walifika kwa wananchi kutoa elimu juu ya namna  ya matumizi  salama ya huduma za  Kibank ili kuweza kuzuia uhalifu kuweza kutendeka ikiwa ni pamoja na kuwa makini na miamala ya fedha wanayoifanya kwa njia yoyote  ile, kutokugawa nambari ya siri ya kadi yake na kutokutoa taarifa zao za siri za kibank kwa watu wengine.
 Jeshi la Polisi kitengo cha Polisi Jamii kutoka Polisi Makao Makuu Dar es salaam likiongozwa na Naibu Kamishina wa Polisi  DCP Ahmada Khamis, pamoja na Maafisa kutoka Bank ya CRDB wametoa elimu kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi Wilaya ya Ruangwa kata ya Nkowe  juu wa wizi wa fedha katika  mitandao na matumizi salama ya huduma mbalimbali za kibank.
 Naibu Kamishina wa Polisi  DCP Ahmada Khamis akitoa  elimu kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi Wilaya ya Ruangwa kata ya Nkowe  juu wa wizi wa fedha katika  mitandao na matumizi salama ya huduma mbalimbali za kibank.
Afisa kutoka Bank ya CRDB akitoa elimu kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi Wilaya ya Ruangwa kata ya Nkowe  juu wa wizi wa fedha katika  mitandao na matumizi salama ya huduma mbalimbali za kibank.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...