Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KWA Ujinga wangu naomba niseme mapema tu, mimi si mfanyabiashara ila 
nimekuwa karibu kwasababu nanunua bidhaa za wafanyabishara.

Nanunua bidhaa za wafanyabishara kulingana na mahitaji yangu ya kila 
siku.Ndio ukweli maana maisha yangu ni kwamba nikijipata vijesenti naenda dukani nanunua nachojitaji.Kwa kuwa nimekuwa karibu na wafanyabishara , nikiri nimekiwa nikifuatilia 

mambo yao mbalimbali.Hata wanapotoa malalamiko yao kuhusu kukwamishwa kwa mambo yao nimekuwa nikisia.Malalamiko ya tozo kubwa za kodi kwenye masuala ya biashara nayo nimekuwa nikiwasikia wafanyabishara wakilalamika.

Nawasikia kwasababu mbali ya kuwa ni sehemu ya mteja wao , bado nami ni Mtanzania ambaye nashukuru Mungu ni muumini wa kufuatilia kila jambo nchini kwetu.Hata Rais wangu Dk.John Magufuli wakati unatoa maagizo kwa Waziri wa Fedha na Mpango kukaa na Mamalaka ya Mapato Tanzania(TRA)kuangalia namna ya tozo za kodi.

Ukasema kuwa kodi zimekuwa kubwa kiasi cha kufanya kuwa kero.Ukaeleza 
namna ambavyo unataka kodi iwe jambo la heshima kwa Taifa na si kuwa kero kwa mlipaji.Kwa Ujinga Wangu baada ya kusikia utakutana na wafanyabishara kutoka maeneo mbalimbali nchini.Nikasema kwenye mazungumzo hayo lazima kitaeleweka.

Rais Magufuli ukaamua kutoa nafasi ya kila mfanyabishara kutoa dukuduku lake.Nakumbuka kwenye mkutano huo ambao wewe uliongoza ulieleza namna ambavyo unataka kumsikia kila mmoja wao.Wafanyabishara nao kwa kuwa kuna mambo ambayo yalishikuwa kero kwao waliamua kusema kila kitu.Hakuna ambacho wamekificha maana waliona ndio sehemu pekee ya wao kusikilizwa.

Wakaeleza changamoto ambazo wanakutana nazo kutoka kwa TRA.Wakaeleza namna ambavyo wanaojihusisha na biashara ya mazao kuharibikia njiani.Wakaeleza namna ambavyo wanatamani Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya biashara.

Wafanyabishara hao wakaelezea mambo mengi.Wakaeleza namna ambavyo wanaamini kikao hicho kati yao na Rais kitakuwa na mafanikio makubwa.Kama nilivyotangulia kueleza awali mimi si mfanyabiashara lakini nimevutiwa na mazungumzo kati ya pande hizo mbili.
 Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  alipokuwa akiendesha  mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam hivi karibuni .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...