KAMPUNI ya kutengeneza mvinyo ya Moët & Chandon imetambulisha kilaji  kipya cha kampuni hiyo cha Moët Nectar Imperial, uzinduzi ambao umefanyika na balozi wa kinywaji cha Moët & Chandon, Pierre-Louis Araud.

Akizungumza wakati wa kutambulisha kinywaji hicho Balozi wa kinywaji cha Moët & Chandon Pierre-Louis Araud amesema kuwa ni kinywaji chenye uhai na ukarimu, kikiwa na rangi ya njano iliyong'arishwa na dhahabu na kinajitofautisha na vingine kwa ustadi na utajiri wake  wa ladha.

Amesema kuwa "Urafiki, ushirikiano na ukarimu" ni kati ya maadili ya chapa ya Moët. Moët & Chandon inashiriki katika kuunganisha watu ulimwenguni kote na kujenga urafiki wa kudumu. Tunapofurahia uzinduzi wa Moët Nectar nchini Tanzania, pia tunataka kusheherekea watanzania kama marafiki wapya wa Moët na tunaendelea kuwapa moyo wale wote wanaopenda kufurahia maisha kushukuru kwa kila wakati na kusheherekea mafanikio kila yanapotokea." 

Harufu ya Moët Nectar Impérial ina wingi wa matunda ya kitropiki kama mananasi na maembe, viungo vitamu vya mdalasini na vanila. Kikiwa mdomoni kina mchanganyiko wa ladha nzuri ya krimu na mazabibu.

Mchanganyiko wa kinywaji cha Moët Nectar Impérial unajengwa kwenye muundo wa zabibu ya aina mbali mbali ikiwemo wa aina ya Pinot Noir (asilimia 40 kwa 50), pia aina ya Meunier (30 kwa 40) na pia aina ya Chardonnay kwa asilimia (10 kwa 20). Matumizi ya asilimia 20 hadi 30 ya mvinyo ambayo imehifadhiwa kwa uangalifu yanakamilisha uundaji wa kinywaji hiki na kukiboresha zaidi. 
Balozi wa kinywaji cha Moët & Chandon Pierre-Louis Araud akionesha kinywaji cha Moet & Chandon ambacho ni Moët Nectar Imperial ambacho kimetambulishwa jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Kinywaji cha Moët & Chandon Tanzania.
 Balozi wa kinywaji cha Moët & Chandon Pierre-Louis Araud  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutambulisha kinywaji cha Moet &Chandon cha Moët Nectar Imperial hapa nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Kinywaji cha Moët & Chandon Tanzania na kushto ni Meneja Masoko wa Kinywaji cha Moët & Chandon hapa nchini, Alexandre Kelaine.
 Balozi wa kinywaji cha Moët & Chandon, Pierre-Louis Araud  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutambulisha kinywaji cha Moët Nectar Imperial hapa nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Kinywaji cha Moët & Chandon Tanzania na Kutoka kushoto ni  Meneja wa Chapa (Band) wa Kinywaji cha Moët & Chandon na Kulia Meneja Masoko Afrika Mashariki wa  Moët Hennessy, Alexandre Helaine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...