Na Zainabu Nyamka,Globu ya jamii

MBUNGE wa Jimbo la Nyamagana  Stanlaus Mabula ameweka mkakati wa kuibua, kukuza na kuendeleza mpira wa wavu ili  uwe ajira. 

Mabula amebainisha haya  leo kwenye uzinduzi wa Mpira wa Wavu wenye jina la Mrajam Volleyball Championship inayohusisha  vikosi nane kutokea Mwanza, Zanzibar, Manyara, Mara,  Shinyanga na kilele chake kuwa Machi 25/mwaka huu.

Akiwakilishwa na Ahmed Misanga kwa niaba yake amesema mbunge wa Nyamagana amefarijika michuano hiyo kuja kufanyikia Nyamagana na kuweka historia kuwa michuano ya kwanza kufanyika katika uwanja uliozinduliwa wiki mbili zilizopita. 
"Mchakato wote wa upatikanaji wa wadau wa maendeleo ulitokana na jitihada zake na kuwezesha kujengwa uwanja huo uliogharimu Sh. 122,000,000.Amewaambia waandaaji ni heshima kubwa kupata mwaliko huo adhimu  na yupo tayari kushirikiana na vilabu vya mpira wa wavu jimboni humu kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji hivi na kuwa ajira.

Amefafanua  ofisi ya Mbunge wao ipo wazi,hivyo waende wakazungumze na kuweka  mkakati wa pamoja wa kudumu utakaokuwa chachu ya kuibua vipaji vya mpira wa Wavu, kuviendeleza na kuwa ajira ndani ya wilaya,  kimkoa, kitaifa na kimataifa.

" Maana kiu na furaha yangu nikuona mchezo wa wavu unakuwa ni zaidi ya mazoezi ya mwili bali unakuwa ajira,"amesema.Uzinduzi huu leo umezinduliwa na mgeni rasmi  Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha aliyewakilishwa na Ofisa tawala.  

Wageni wengi ni ofisi ya Mbunge Ilemela iliyowakilishwa na Micheal Goyele, Wenyeviti wa Ilani vya mpira wa wavu Mwanza,  Tabora,  Mara. Vikosi vinane vinavyochuana nipamoja na:, Nyuki Zanzibar, Polisi Zanzibar, Ngorongoro Manyara, MTC jeshi Mwanza, Magu, Bunda, Shinyanga pamoja na kikosi kutokea Chuo kikuu cha Mtakatifu Augustine Mwanza. 

Mshindi wa kwanza ataibuka na kitita cha shilingi million moja, mshindi wa pili atapata shilingi laki tano na mshindi wa tatu atapatiwa shilingi laki mbili. Wachezaji sita bora wataondoka navyeti pamoja na elfu 30.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...