Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii

KAMATI ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Chama Cha Mapanduzi(UVCCM) imemtema Jokate Mwegelo kwenye nafasi ya kaimu Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji wa jumuia hiyo uanzia leo.

Uamuzi huo umetolewa leo Mjini Dodoma huku sababu za kuondolewa kwake zikiwa hazijawekwa bayana.

Akizungumza na Michuzi Blog kwa njia simu ya mkononi akiwa mkoani Dodoma,Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka amesema Jokate ameondolewa kwenye nafasi hiyo ambayo kimsingi alikuwa anaikamu na ameitumikia kwa mwaka mmoja.
Amesema kwa mujibu wa Katiba ya UVCCM ,Baraza Kuu la jumuiya hiyo ndio lenye jukumu la kuteua jina kwa ajili ya kulipendekeza na kulipitisha kwenye nafasi hiyi lakini Jokate alipata nafasi hiyo kupitia Kamati ya Utekelezaji.
Amesema hawezi kusema ni sababu gani ambayo imesababisha aondolewe lakini moja ni hiyo ya kwamba wenye uwezo wa kupitisha jina kwenye nafasi hiyo ni Baraza Kuu na yeye aliipata kupitia Kamati ya Utekekezaji.

Ameongeza ifahamike Jokate alikuwa anakaimu tu nafasi hiyo na unaweza kuilezea kama alikuwa bado kwenye majaribio ,hivyo nafasi hiyo itajazwa baada ya Baraza Kuu Kukutana kwenye kikao chake kwani leo haikikuwa kikao cha baraza.
"Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM ndio iliyotoa uamuzi huo na si  Baraza Kuu la jumuiya yetu.Kamati hiyo ndio ilimkamisha nafasi hiyo na ndio iliyomuondoa," amesema Shaka.
Alipoulizwa sababu za msingi za kumuondoa kwenye nafasi hiyo ni zipi?Shaka amejibu ni mapema kusema sababu   ila kikubwa alikuwa anakaimu nafasi hiyo na sasa ametenguliwa.
"Ujue unapokuwa umakaimu nafasi inakuwa ni kipindi cha majaribio na lolote linaweza kutokea aidha kuthibitishwa kwenye nafasi unayokaimu au kutothibitishwa," Shaka.
Kuhusu kikao cha leo amefafanua hakikuwa kikao cha Baraza Kuu la UVCCM bali ilikuwa ni semina elekezi kwa vijana wa jumuiya hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...