Na Leandra Gabriel, globu ya jamii

WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe leo Machi 29 ametoa tamko kuhusu wasanii waliofungiwa kazi zao za sanaa.

Akizungumza jijini Dar es salaam Dk.Mwakyembe ameeleza kuwa Serikali haina ugomvi na msanii yeyote ila ugomvi wao upo katika suala la mmomonyoko wa maadili na suala hilo halitofumbiwa macho, pia ameeleza kuwa kuna mipaka katika kulinda maadili na wasanii ndio mabalozi, kuhusu suala la Abdul Naseeb maarufu kama Diamond la kutoa kauli nzito mtandaoni Mwakyembe amesema kuwa wanampenda sana Diamond na wanataka afike mbali zaidi na amefurahi sana kwani vijana hao wameelewa.

Akieleza maamuzi hayo naibu Waziri wa wizara husika Juliana Shonza amesema hawana ugomvi wala chuki na msanii wa Tanzania na kuhusu suala msanii Suzan Michael maarufu kama Pretty kind amesema amefurahishwa na hatua alizochukua kama kujisajili katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wanaamini amebadilika hivyo wanamsamehe adhabu yake iliyotakiwa kuisha Julai Mosi mwaka huu.

Pretty kind ameshukuru Wizara pamoja na Baraza la sanaa la taifa (BASATA) kwani kupitia wao amejifunza mengi na atakuwa balozi mzuri wa maadili nchini na amewashauri wasichana hasa wasanii kufuata sheria na kanuni zilizowekwa na BASATA na wabadilike kupitia yeye.Kuhusu suala la Roma Mkatoliki, Shonza ameeleza kuwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lilimpa maelekezo ya mabadiliko ya wimbo wa kibamia na kuhudhuria kikao kilichopangwa na Baraza hilo vitu ambavyo Roma hakuvitekeleza.

Aidha Shonza ameeleza kuwa Roma aliandika barua ya kupunguziwa adhabu ombi ambalo wamelipokea ila lazima akajisajili BASATA pamoja kufanya marekebisho ya wimbo huo.Baada ya msanii Roma kuamua kwa ridhaa yake mwenyewe mbele ya vyombo vya habari kwamba wimbo huo uondolewe kabisa kwenye vyombo vya habari hasa kwa mfumo wa sauti na video Waziri Mwakyembe amesema kuwa pindi atakapokamilisha usajili wake na kuwa na hati kutoka BASATA adhabu yake itakuwa imeishia hapo.

Mwisho waziri Mwakyembe amewaomba wasanii kuwa mabalozi wa maadili ya watanzania kwa kumnukuu baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere kwa kusema Taifa lisilo na maadili yake ni taifa mfu.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe na Naibu wake, Juliana Shonza (katikati mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii hao baada ya kuongea na wanahabari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...