Viongozi wa taasisi za elimu ya juu nchini ambazo wanafunzi wake wanapokea fedha za mikopo kutoka Serikalini kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafuzi wa Elimu ya Juu (HESLB) zimetakiwa kuwawezesha maafisa wanaosimamia madawati ya mikopo katika taasisi hizo ili watoe hudima bora kwa wanafunzi.

Akifunga kikao kazi cha siku mbili kati ya Menejimenti ya HESLB na maafisa wanaosimamia madawati mikopo kutoka taasisi za elimu ya juu zaidi ya 70 mwishoni mwa wiki mjini Morogoro, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo amewataka viongozi wa taasisi hizo kuhakikisha maafisa wao wana vitendea kazi vya uhakika na wanapata ushirikiano wa kutosha.

Madawati hayo ya mikopo yalianzishwa mwaka 2011 katika taasisi zote za elimu ya juu kufuatia maelekezo ya Serikali ili kuongeza ufanisi katika kusimamia shughuli za utoaji mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi.  
“Kila mdau kwenye utoaji wa mikopo ya elimu ya juu ana wajibu wake, Serikali inatoa fedha kwa wakati na menejimenti za taasisi za elimu ya juu ni wajibu wao ni kuimarisha wadawati ya mikopo yanayowahudumia wanafunzi kwa kuwawezesha ili ninyi maafisa mnayoyasimamia mtoe huduma nzuri kwa wanafunzi … mpewe ushirikiano na vitendea kazi,” alisema Dkt. Akwilapo wakati akifunga kikao kazi hicho kilichofanyika Alhamisi na Ijumaa ya wiki iliyopita (Machi 8-9, 2018).

Dkt. Akwilapo aliwakumbusha maafisa hao kuwa wao ndiyo watu wanaokutana na wanafunzi kwa mara ya kwanza huko vyuoni na kwamba ni muhimu wakatoa huduma bora kama Serikali ilivyotarajia wakati inatoa maelekezo ya kuanzishwa kwa madawati hayo.

Pamoja na kuimarisha madawati ya mikopo, Katibu Mkuu pia amazitaka taasisi kuhakikisha fedha za mikopo ya wanafunzi zinazopelekwa vyuoni zinawafikia wanafunzi kwa wakati kama ilivyokusudiwa na pale ambapo mwanafunzi hayupo chuoni, zirejeshwe kwa Bodi ya Mikopo haraka kama miongozo inavyotaka.
Lengo la kikao kazi

Akizungumza kabla ya Katibu Mkuu, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru alisema HESLB huandaa kikao kazi kama hicho mara moja kila mwaka ili kujadiliana kwa pamoja kuhusu utendaji kazi wetu kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kutoa huduma kwa wanafunzi na wadau wengine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...