Wakulima 2000 kutoka  vijiji sita vya Kata ya Kiru Wilayani Babati wameongeza kipato kutokana na ujenzi wa daraja lililojengwa na Mradi wa Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za kifedha Vijijini (MIVARF),  ikiwa ni sehemu ya malengo ya mradi huo katika kuongeza kipato nchini hususan  maeneo ya vijijini.

Wakulima hao wa Kata ya Kiru, inayojumuisha kaya 306, walishindwa kuongeza kipato kwa takribani  miaka 38,  tangu mwaka 1978, baada ya Daraja walilokuwa wanatumia kusombwa na Mafuriko hadi mwaka 2016, Serikali kupitia Mradi wa MIVARF ilipojenga  Daraja hilo ambalo limeanza kutumika sasa na  kuchochea shughuli zao za  kiuchumi .

Akiongea  na timu ya  wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na  Mradi  wa MIVARF mara baada ya kutembelea Kijiji cha Masware lilipojengwa Daraja hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Babati Hamis Malinga amesema, Serikali kupitia Mradi wa MIVARF imeweza kuchochea uwekezaji katika kata hiyo

“Kiwanda cha Sukari cha Manyara kimeweza kuongeza uzalishaji kutoka tani 15 hadi 30 kwa siku kutokana na ujenzi wa daraja la kijiji cha Masware ambalo limesaidia kuboresha biashara baina ya vijiji na kuongeza kipato kwa wananchi. Aidha, Usafirishaji wa mazao na bidhaa ulikuwa wa gharama kubwa sana lakini kwa jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kupitia mradi huu tumeweza kuona maendeleo makubwa katika Vijiji hivi”, alisema Mkurugenzi Malinga.
Muonekano wa Daraja la Masware lililopo katika kijiji cha Masware Kata ya Kiru Wilayani Babati, daraja hilo limejengwa na Mradi wa Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za kifedha Vijijini (MIVARF).


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...