Na Dotto Mwaibale, Mvomero-Morogoro.

WANAFUNZI wa Shule ya Msingi ya Mvomero mkoani Morogoro wametakiwa kujikita zaidi katika masomo ya Sayansi ili waweze kulisaidia taifa katika nyanja mbalimbali ikiwemo kufanya utafiti.

Mwito huo umetolewa wilayani humo leo na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Shabani Hussein wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la mbegu ya mahindi ya Wema E2109 inayostahimili ukame iliyotolewa na COSTECH kupitia Jukwaa na Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB)

"Ninyi wanafunzi nawaomba someni sana masomo ya sayansi ili hapo baadae muweze kuwa watafiti wa masuala mbalimbali jambo litakalosaidia taifa" alisema Hussein.Alisema tafiti zozote zinafanywa na wataalamu waliobobea katika masomo sayansi hivyo aliwataka wanafunzi hao kujifunza kwa bidii masomo hayo ya sayansi.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya hiyo, Mohamed Utalli aliishukuru COSTECH na OFAB kwa kupeleka mradi huo katika wilaya yake ambapo amewataka wananchi kuzichangamkia mbegu hizo.
Mtifiti Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu ambao ndio waliofanya utafiti wa mbegu hiyo, akitoa maelezo ya jinsi ya kupanda mbegu hiyo.
Uzinduzi wa shamba darasa katika shule ya msingi Mvomero.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mohamed Utalli akizindua shamba darasa kwa kupanda mbegu hiyo ya Wema 2109
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mohamed Utalli, akizungumza na wakulima wanaounda kikundi cha Tupendane kilichopo Kijiji cha Didamba.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Tupendane cha Kijiji cha Didamba, Mwanahamisi Omari (kushoto), akikabidhiwa mbegu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...