Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisaini mkataba wa Makubaliano ya kulifanya Bara la Afrika kuwa eneo huru la Biashara, kwaniaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Machi 21, 2018, jijini Kigali, Rwanda. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU.
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amepongeza makubaliano yaliyofikiwa na nchi za Afrika za kulifanya bara hilo kuwa eneo huru kibiashara.

Majaliwa aliyasema baada ya kumaliza kusaini mkataba wa nchi za Afrika kuhusu mkataba huo akimwakilisha Rais John Magufuli Jijini Kigali ambapo alisema Tanzania imeajiandaa vya kutosha kutekeleza mkataba huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Kigali , Waziri Mkuu alisema Tanzania itahakikisha mkataba huo unatelekezwa bila kuathiri huduma zinazozalishwa ndani.Alisema Tanzania itahakikisha mikataba mitatu ambayo imesainiwa inatekelezwa bila kuathiri uzalishaji na sera za ndani.

Mikataba iliyosaioniwa na mataifa hayo 50 ya Bara la Afrika ni pamoja na mkataba wa kulifanya bara la Afrika kuwa eneo huru la biashara, Itifaki ya kisheria ya utekelezaji wa makubaliano hayo ikiwamo uhuru wa makazi, haki ya kuishi na kufanyakazi popote bila vikwazo wala vizuizi vyoyote.

Azimio la tatu ni Azimio la Kigali ambalo limejumuisha mawazo ya uanzishwaji wa mchakato huo.“Nichukue fursa hii kumpongeza Rais wa Rwanda na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Paul Kagame kwa kutilia maanani suala hili hadi kufikia hatua hii ya kusaini mkataba.

“Tanzania kama wadau wakuu wa mkataba huu tunakwenda kujipanga kuhakikisha mkataba huu unatekelezwa bila kusababisha vikwazo vyovyote.
“Hata hivyo tunakwenda kupeleka baadhi ya masuala haya katika vikao vya Baraza la mawaziri ili kuangalia sheria zetu zisije kuwa kikwazo katika utekelezaji wa mkataba huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...